We have 152 guests and no members online

DRC; WAGONJWA 12 WAJERUHIWA KWA VISU WAKIWA HOSPITALI

Posted On Wednesday, 07 February 2018 04:11 Written by
Rate this item
(0 votes)

media

Watu wasiojuliana wameripotiwa kujipenyeza katika hospitali maarufu katika kata ya Ndosho, mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na kuwachoma visu wagonjwa 12 wakiwa wodini.

Katika mahojiano maalum na shirika la habari la RFI, waziri wa afya katika jimbo la Kivu ya kaskazini Dokta Martial Kambumbu amethibitisha kuwa ni tukio ambalo lilifanyika usiku wa kuamkia jana Jumanne ambapo majambazi hao walivivamia vituo viwili vya afya nje kidogo ya jiji la Goma, ambako walianza kuwachoma visu wagonjwa ambao walikuwa wamelazwa wakipewa matibabu. Pamoja na kukiri kuwa majeruhi hao wanaendelea vizuri waziri Kambumbu ameongeza kuwa watatu kati ya wagonjwa hao wako mahututi.

Mashirika ya kiraia katika mji huo wa Goma yanasema hali hiyo imezusha hofu ya kuwepo kwa waasi wa Uganda wa ADF wanaouwa watu kwa kutumia visu katika maeneo ya Beni na viunga vyake.

Read 65 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu