We have 155 guests and no members online

JIFUNZE KUPITIA NENO LA LEO; MWANA WA GAVANA ANAPOTENDA KOSA.

Posted On Wednesday, 07 February 2018 04:46 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image may contain: 1 person, standing and outdoor

Na MAGGID MJENGWA.

Kuna kisa cha mwana wa gavana katika Misri ya kale. Mwana yule alitembea akijivunia cheo cha baba yake.akajawa kiburi kufikia siku moja kumdhalilisha mwalimu wa shule mtaani huku watu wazima na watoto wengine wakiangalia. Ndio, mwana yule alimchapa bakora ya matakoni mwalimu yule, tena hadharani. Mwalimu alifedheheshwa sana, maana hata kosa hakulijua. Mwalimu yule akafunga safari ndefu kwenda kuarifu jambo lile kwa mfalme wan chi. Huko akapokelewa, akaeleza yaliyomsibu.

Mfalme akaamuru mwana yule wa gavana aletwe haraka kujibu shauri akiambatana na baba yake, yaani gavana mwenyewe. Baada ya kusikiliza shauri lile, mtawala yule akajiridhisha kuwa mwana yule wa gavana allitenda kosa. Akamwamuru mwalimu yule achukue bakora na kumchapa mwana yule wa gavana bakora mbili za matakoni.

Mwalimu aliinua bakora akaanza; moja, ikaja ya pili. Akatamka, “Mfalme wangu nimemaliza”. Mfalme akasema, “Bado, chukua tena bakora mchape gavana bakora tatu za matakoni”. “Ewe mfalme wangu, gavana hajanitendea kosa lolote, ni mwanae” alitamka mwalimu yule.

Mfallem akamwambia “Nimekwambia mchape gavana bakora tatu kwa kuwa bila ya yeye, mwanae asingetenda kosa hilo”

Hili ndilo neon la leo.

Na Maggid Mjengwa

Read 106 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu