We have 157 guests and no members online

PAKISTAN; MAHAKAMA YATOA ADHABU YA KIFO KWA ALIYEMCHOMA MWANAFUNZI.

Posted On Thursday, 08 February 2018 05:24 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for LAW

Mahakama nchini Pakistan imemhukumu mwanume mmoja adhabu ya kifo na kuwatia hatiani wengine 30 kuhusiana na tukio la kuchomwa kwa mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 23 aliyetuhumiwa isivyokweli kukashifu dini.

Mohammad Mashal Khan aliuwawa na kundi la watu katika chuo kikuu alichokuwa akisomea mnamo Aprili 2016 kutokana na tetesi ambazo baadae zilithibitishwa kuwa za uongo kwamba alisambaza kwenye mitandao ya kijamii ujumbe uliokuwa unakashifu dini. Kutoa kauli za kuukashifu Uislamu nchini Pakistan ni kosa linalobeba adhabu ya kifo na madai tu yanatosha kusababisha umati wa watu wakamvamia mtuhumiwa. Mahakama hiyo ya kupambana na ugaidi baada ya kutoa hukumu hiyo ya kifo imetoa hukumu ya kufungwa maisha kwa watu wengine watano huku wengine 25 wakifungwa kwa miaka minne na watu 26 wameachiliwa huru baada ya kukosekana ushahidi.

Read 39 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu