We have 154 guests and no members online

MAKUNDI YA KIGAIDI SUDANI KUSINI YAWAACHIA WATOTO 311.

Posted On Thursday, 08 February 2018 12:38 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for the return of child soldiers in south sudan

Umoja wa mataifa umetangaza kuachiliwa kwa watoto zaidi ya 311 kutoka kwenye makundi ya kigaidi nchini Sudani Kusini. Kundi hilo la watoto linahusisha wasichana 87 ambao sasa watajiunga na jamii zao kuendelea na maisha mapya ya uraiani. 

Mjumbe wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini David Shearer, amesema Idadi ya wasichana hao walioachiliwa ni kubwa zaidi na ni kwa mara ya kwanza kufikiwa katika matukio ya kurejeshwa kwa watoto wanaohusishwa na ugaidi. Kadhalika amesema wengine wamekuwa wakirejeshwa baada ya kufanyiwa ukatili wa kingono, lakini waliorejeshwa hawakubainika kuwa na matatizo.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na umoja wa mataifa, katika mikakati ya kupigania uhuru wa Sudani kusini, watoto 563 walifunzwa mafunzo ya kijeshi, na kati yao watoto 137 walijiunga na jeshi la kupigania wananchi upande wa upinzani.

Sudan kusini ilianzishwa mwezi julai mwaka 2011, baada ya kujipatia uhuru uliotokana na kugawanywa kwa sudani Kusini na Kaskazini. Baadae taifa hilo lilitumbukia katika migogoro mwezi December mwaka 2013, yalidaiwa kufadhiriwa na aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar. 

Shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa UNICEF, linasema pande zote mbili za sudani kusini na sudani kaskazini, zinawatumia watoto katika mapigano. 

Tangu kuanza kwa mapigano hayo, watu makumi elfu wameuwawa, huku wengine wanaokadiriwa kuwa robo ya wananchi wote wa sudani kusini, wakirazimika kuyahama makazi yao.     Ripoti nyingine za umoja wa mataifa zinasema, watu milioni sita ambao ni nusu ya wananchi wote, wanahitaji misaada ya kibinadam huku wengine zaidi ya milioni 1.2 wakisumbuliwa na njaa.

 

Read 42 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu