We have 159 guests and no members online

MPANGO WA KUBADILI KATIBA YA BURUNDI WAPINGWA NA KATIBU MKUU WA UN.

Posted On Thursday, 08 February 2018 14:33 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for antonio gutierrez

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekosoa jaribio la rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kutaka kubadilisha katiba ya nchi hiyo hatua ambayo itamruhusu kukaa madarakani kwa muongo mwingine au zaidi. Katibu mkuu Guterres amesema upinzani na mashirika ya kiraia ni lazima yashirikishwe kwenye maamuzi yoyote ya kubadili katiba ili kuzuia uwezekano wa nchi hiyo kutumbukia kwenye mzozo zaidi.

Guterres ameongeza kuwa anatambua Burundi kama nchi inayo mamlaka ya kujiamulia mambo yake kama taifa huru lakini akaonya kuwa jambo la kubadili katiba linahitaji maridhiano ya pande zote.

Wakati huo huo muungano wa wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni nje ya nchi CNARED unaendelea kulaani jaribio lolote la kubadili katiba, ukibaini kwamba hali hiyo itaitumbukiza Burundi katika machafuko, zaidi ya yale yaliyotokea tangu mwaka 1993 hadi 2004.

Toka mwaka 2015 nchi ya Burundi imeshuhudia vurugu zilizosababisha maelfu ya raia kukimbia nchi yao baada ya rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula watatu na kusababisha machafuko.

Read 42 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu