We have 159 guests and no members online

WALIOPOTEZA MAISHA KWENYE TETEMEKO CHINA WAFIKIA 9 TOFAUTI NA ILIVYOTANGAZWA AWALI.

Posted On Thursday, 08 February 2018 15:11 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for china earthquake

Timu za waokoaji katika eneo la mashariki mwa nchi ya Taiwan zimeendelea Alhamisi hii kuchimba vifusi vya jengo la makazi lililoporomoka baada ya tetemeko la ardhi la Jumanne. Maafisa wa idara ya zima moto kwenye kisiwa hicho wamesema kuwa idadi ya vifo hadi sasa imefikia watu 9 na sio 10 kama taarifa za awali zilivyoripoti. Pia wamefafanua kuwa idadi ya watu wasiojulikana mahali walipo imeshuka kutoka 60 hadi 10.

Takriban watu watatu miongoni mwa waliokufa ni kutoka China. Jengo hilo la ghorofa 12 na ambalo ni maarufu kwa watalii liliharibiwa vibaya na tetemeko hilo lenye nguvu ya 6.4 katika kipimo cha rikta. Zaidi ya watu 250 walijeruhiwa kwenye tukio hilo ambalo pia liliacha majengo mengine matatu ya ghorofa yakiwa yameinama ikiweko hoteli ya Marshal ambapo watu wawili walikufa. Zaidi ya watu 800 walikesha kwenye mehema wengi wao wakiogopa kurudi nyumbani kwa kuhofia kurudi tena kwa tetemeko hilo.

Read 39 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu