We have 178 guests and no members online

MAHABUSU 13 WAACHIWA NA BOKO HARAM

Posted On Sunday, 11 February 2018 15:21 Written by
Rate this item
(0 votes)

Image result for boko haram release 13 prisoners

Wanamgambo wa Boko Haram wamewaachia huru mahabusu 13 kaskazini mashariki mwa Nigeria.Walioachiwa huru ni pamoja na wasichana 10 waliotekwa nyara mwezi Juni uliopita, pamoja na wataalam watatu wa jeolojia kutoka chuo kikuu cha Maiduguri.

Habari hizo zimetangazwa na msemaji wa ikulu ya rais, Garba Shehu. Wataalamu hao wa chuo kikuu walikuwa sehemu ya kundi la wataalam walioanza kufanya utafiti wa mafuta katika eneo linalopakana na ziwa Chad. Watu wasiopungua 69 waliuwawa kufuatia shambulio hilo, linaliotajwa kuwa la kikatili kabisa kuwahi kushuhudiwa mwaka 2017. Serikali ya Nigeria ilijadiliana na kundi hilo la magaidi kabla ya mahabusu hao kuachiliwa huru. Msemaji wa rais hakusema lakini kama kuna pesa zilizotolewa au kama mahabusu hao wamebadilishwa na wafuasi wa Boko haram waliokuwa wakishikiliwa. Shirika la klimataifa la Msalaba Mwekundu ambalo linashughulikia kurejeshwa nyumbani mahabusu, halijashiriki katika mazungumzo kati ya serikali ya Nigeria na Boko Haram.

Read 86 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu