We have 175 guests and no members online

BI. ELEN SIRLEAF ASHINDA TUZO YA MO IBRAHIM

Posted On Monday, 12 February 2018 04:49 Written by
Rate this item
(0 votes)

 Related image

Ellen Johnson Sirleaf Rais wa zamani wa Liberia ameshinda tuzo ya mwaka ya Mo Ibrahim kwa Uongozi wa Afrika  ambayo hupewa viongozi wa Afrika  wanaoonekana kuwa na utawala mzuri. Tuzo hiyo ilianzishwa na Mo Ibrahim Mjasiriamali Mwingereza mwenye asili ya Sudan mnamo mwaka 2007 kwa ajili ya kuwatunuku viongozi walioonesha kazi nzuri wakati wa kipindi cha uongozi wao ndani ya bara la Afrika.

Ikumbukwe kuwa Ellen Johnson Sirleaf amekuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kushika nafasi ya Urais mwaka 2006 na kumaliza muda wake mwezi uliopita baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

Kamati ya Utendaji ya tuzo ya Mo Ibrahim imesema Ellen Johnson Sirleaf ameonesha uongozi wa kipekee katika kukabiliana na changamoto zisizowahi kutokea katika awamu zake mbili za uongozi alipokuwa Rais wa Liberia.

Wakati aliposhinda uchaguzi wa Rais nchini humo mwaka 2005, nchi hiyo ilikuwa imegawanyika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka kadhaa na tuzo hiyo ya amani ilikuwa ni kwa ajili ya kumpongeza kusaidia kuiimarisha nchi hiyo.

Wakosoaji wake wamekuwa wakimkosoa kwa kuwa na upendeleo, kutokana na kuwachagua watoto wake katika nafasi za ngazi za juu na pia wanadai kuwa hakuchukua hatua za kutosha kupambana na rushwa.

Kamati yab utendaji ya Mo Ibrahimu imearifu kwamba inafahamu mapungufu yake, lakini imeamua kwamba anastahili kupata tuzo ya dola za kimarekani milioni 5.

Tuzo hii ambayo inapaswa kutolewa kila mwaka , kwa mara sita mfululizo ilishindwa kupata mtu, kutokana na viongozi kukosa sifa za kushinda tuzo hiyo.

Ellen Johnson Sirleaf atapata dola za Kimarekani milioni tano zitakazogawanywa kwa miaka kumi, na dola laki mbili kwa maisha yake yote.

 

Read 87 times

Add comment


Security code
Refresh

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu