We have 958 guests and no members online

mjengwablog

mjengwablog

Saturday, 25 February 2017 04:21

Tuweke Tahadhari Kwa MV.Kigamboni...

Picha ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,
Jana majira ya saa tisa na nusu alasiri, nahodha wa MV. Kigamboni ambapo nami nilikuwa abiria, alilazimika kusimamisha chombo katikati ya safari kuruhusu fundi anyanyue lango la mbele lililoteremka na kugusa maji.
MV. Kigamboni hata kwa macho tu inaonekana imechakaa na inayohitaji ukarabati.
Wahusika wachukue tahadhari badala ya kusubiri maafa yatokee kwanza.
Maggid.

Saturday, 25 February 2017 04:20

MAWAZIRI WA SMZ WATEMBELEA WIZARA YA ARDHI

LUK1

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwaelezea Mawaziri kutoka Zanzibar jinsi Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kinavyorahisisha kutoa Huduma za Ardhi bila usumbufu kwa Wananchi. Kuanzia Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Hamad Rashid, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib na Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila.

RC1

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizindua jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Mkoani Singida, kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina M. Lutambi na kushoto ni Mratibu wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Mkoani Singida Daniel Munyi.

Wa kwanza kushoto mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Magid Mwanga ,wa pili kushoto mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo na Jack Feng mkurugenzi wa kiwanda, wa tatu kushoto ni waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage na Ridhiwan Kikwete na Cliford Tandari wakiweka udongo kwenye jiwe la msingi.(picha zote na Mwamvua Mwinyi)

mah1

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati Ndogo ya Mawaziri wa Siasa na Diplomasia wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Mkutano huo umefanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Saturday, 25 February 2017 04:12

Aonavyo Mwenyekiti Wenu...

Hakuna Ugumu Wa Kuhama Kwenye Viroba Na Kuhamia Kwenye Mananasi...
Ukizingatia kiroba ni elfu moja na nanasi mia tano...
Pichani ni Kivukoni, jana jioni.

Friday, 24 February 2017 09:41

Swali La Kizushi... Mkapa Yanga Au Simba?

Picha ya Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

Kesho ni siku ya Ngoma Kuu. Ni Simba na Yanga.

Katika utawala wake, Benjamin Mkapa hakupata kuonekana kwenye viwanja vya soka. Ajabu ya Mkapa, wakati wananchi wake wakitafakari juu watafanyaje na uwanja wao wa taifa uliochakaa, ni Benjamin Mkapa aliyeahidi kuwajengea uwanja wa kisasa kabla hajamaliza muda wake, na akatimiza ahadi yake hiyo.

Friday, 24 February 2017 09:38

Taarifa Kuhusu Utapeli Ajira za JWTZ

media

Waandamanaji waliandamana Alhamisi Nigeria wakiomba kufukuzwa kwa raia wa Afrika Kusini waishio nchini Nigeria wakilipiza kisasi kile kinachotokea nchini Afrika Kusini, Februari 23, 2017.

Page 1 of 2862

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart