We have 70 guests and no members online

mjengwablog

mjengwablog

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefanya kikao na viongozi wa serikali pamoja na watendaji wa Tanesco, REA katika kikao cha maendeleo ya usambazaji umeme kilichofanyika ofisini kwake, Mjini Dodoma 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amekutana na kufanya mazungumzo na wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DR Congo.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli asikitishwa na hafurahishwi na mjadala wa kuongezwa kipindi cha Urais toka miaka 5 iliyowekwa kwa mujibu wa katiba hadi miaka 7.

Mhe. Prof. Palamagamba J. Kabudi (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria akisoma hotuba wakati akimuwakilisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kuwekwa Wakfu Askofu wa Pili wa Dayosisi ya Shinyanga Rev. Can. Capt. Johnson Japheth Chinyong'ole.

 

Ndugu zangu,

Ajabu yetu wanadamu ni pale tunapofunga safari kwenda mbali kusaka miujiza ili hali miujiza tumeibeba kwenye mioyo yetu.

Mwanadamu anapojitambua, akajiamini na hata kuthubutu kutenda, basi, anaweza kufanya miujiza, yeye mwenyewe.

Ni Neno La Leo.

Maggid.

Sunday, 14 January 2018 09:18

Tambaza, Miaka 34 Iliyopita!

 

Ndugu zangu,

Asubuhi ya Jumatatu ile ya tarehe 14 mwezi Januari mwaka 1984 tulikusanyika kuanza Form One pale Tambaza Boys Sekondary School, Upanga, Dar es Salaam.

Haraka sana niliiona familia mpya; Tambaza Family. Wana-Tambaza tuliishi kama ndugu.

Kama wanafunzi, hatukupenda kuonewa, kuonea, na wala kuwaona wanafunzi wa shule nyingine wakionewa .

Kuna mengi niliyojifunza nikiwa Tambaza, kinadharia na vitendo. Naikumbuka Jumamosi moja tukiwa Kidato Cha Pili, mmoja wa walimu wangu, marehemu Mwalimu D. J. Mkomagu aliniachia somo maridhawa. Mwalimu Mkomagu alishiriki kutunga kitabu cha riwaya ya ' Zaka la Damu' akiwa na Harrison Mwakyembe kama kazi ya kitaaluma wakiwa shuleni. Kitabu hicho kikaja kutumika mashuleni.

Ilikuwaje basi Jumamosi ile;

Ni hivi, kuna vyoo vya shule viliziba. Havikutumika kwa muda mrefu. Siku hiyo Mwalimu Mkomagu alitutaka wote tufike shuleni tukiwa na nguo za kazi. Naye alivalia jeans na buti kubwa.

Alitamka;

" Hatuwezi kusubiri Wizara ya Elimu ije kutuzibulia vyoo vyetu. Kazi hiyo tutaifanya wenyewe."

 

Leo tungemwita Mwalimu Mkomagu ' Mzee wa Hapa Kazi Tu'.

Kama utani, Mwalimu Mkomagu aliongoza operesheni ile kwa vitendo. Tulikuwa naye katika kila hatua. Na hakika, ndani ya saa nne, vyoo vile vikazibuliwa na kuanza kutumika.

Kikubwa nilichojifunza kutoka kwa Mwalimu Mkomagu ni kuwa Uongozi si kusimamia tu, bali ni kushiriki kwa vitendo katika kukifanya kile, kama kiongozi, umewataka wengine wafanye.

Nilichokikosa Tambaza? Wasichana.

Ilikuwa ni shule ya wavulana watupu. Naamini, kuwa kwa miaka minne nilikosa mitazamo ya wasichana katika masuala mbalimbali tuliyokuwa tukisoma na kuyajadili. Bila shaka, ingenisaidia mimi na wengine wengi katika kupanua uelewa wa masuala mbali mbali.

Naam, ni wakati wa kutafakari na kujiuliza pia, kuwa hata katika wakati huo, tulikuwa na ndoto gani kwa nchi yetu.

PS: Pichani kutoka kushoto; Shaban Nduku, mimi, Mussa Twaha Kitonge na Ngaja Mussa Mchele.)

Maggid.

Na Tiganya Vincent

SERIKALI Mkoani Tabora imeagiza kukamatwa mara moja wazazi au walezi ambao hadi kufikia Jumatatu ijayo (15, January 2018) watakuwa wameshindwa kuhakikisha kuwa watoto wao waliochaguliwa kujiunga Kidato cha kwanza mwaka huu watakuwa hajaripoti katika Shule walizopangiwa.

media

Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dr Ali Mohamed Shein wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Network Information Centre Mhandisi Abibu R. Ntahigiye (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kampeni ya msafara kwa njia ya barabara (Roadshow Campaign) inayofanywa na taasisi ya Dot tz na Dot africa kuhamasisha matumizi ya mitandao hiyo ya intaneti kwa Afrika leo mkoani Dodoma. Kulia kwake ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Registry.Africa Ndg. Lucky Masilela.

Page 2 of 3135

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi