We have 189 guests and no members online

mjengwablog

mjengwablog

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano  la uwajibikaji kwa mamlaka za  Serikali za mitaa nchini linalotarajiwa kufanyika kuanzia kesho Desemba 5-6,2017 katika hoteli ya Ramada iliyopo Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Magufuli  mapema  leo Desemba 4,2017, amekutana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia nchini Bi. Bella Bird aliyekutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akizungumza wakati Mahafali ya Shule Mikocheni Islamic ambapo aliwaasa wazazi kuwekeza katika kuwapatia watoto elimu ya Duniani na dini hili waweze kuja kuwa watumishi waadilifu baadae pindi wanapokuja kuwa viongozi wa Umma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa kikundi cha Walemavu kutoka Mwembe Makumbi kinachojishughulisha na kutengeneza viatu wakati alipotembelea maonyesho ya walemavu katika uwanja wa Skuli ya Uzini.

  Mjumbe wa Kamati Kuu yaTaifa ya  CCM,  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua mkutano Mkuu wa CCM wa Mkoa wa Lindi kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Nachingwea Desemba 3, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) ametoa mud wa siku 30 kwa wahusika ambao ni wamiliki wa magogo yaliyokamatwa katika bandari ya Dar e s  Salaam ambayo yalikuwa yasafirishwe nje ya Nchi, kujitokeza ili mara moja kueleza wameyato wapi na walikuwa na lengo gani baada ya kuyatelekeza bandarini  hapo kwa muda wa miaka 10 sasa.

Wakazi wa Mkoa wa Tabora wametakiwa kulima mazao ya korosho na mihogo kwa ajili kujiongezea kipato ambacho kitawawezesha kuboresha maisha yao na kujiinua kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwahutubia wananchi wa Kijiji na Kata ya Nyawilimilwa Wilaya ya Geita wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani. 

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya watu wenye ulemavu katika Chuo Cha Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu, Dar es Salaam jana , kulia ni Balozi wa Kuweit nchini Tanzania,  Jasem Al-Najem.

Page 4 of 3115

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji