We have 66 guests and no members online

mjengwablog

mjengwablog

Wednesday, 13 February 2013 04:20

pinda azindua jengo jipya ocean road

 Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akikata utepe kwa kushirikiana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki  Duniani Yukiya Amano (wa pili kutoka kushoto) kuashiria uzinduzi rasmi wa  jengo jipya lenye  vifaa vya kisasa kwa ajili ya  kuwahudumia wagonjwa wa kansa katika Taasisi ya Kansa jana Ocean Road jijini Dar es salaam. Wengine ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto), Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kansa Ocen Road Prof. Twalib Ngoma (wa tatu kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid.

Wednesday, 13 February 2013 04:12

ccm yavuna vijana 2 chadema

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na waliokuwa viongozi waandamizi wa CHADEMA.Kushoto anayevaa kofia ya CCM ni aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Mbozi Magharibi  kwa tiketi ya CHADEMA Bwana Mtela Mwampamba na kulia ni Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana CHADEMA Bi  Juliana Shonza.Wengine katika picha ni Katibu mkuu wa CCMNdugu Abdulrahman Kinana(kulia) na kushoto ni Makamu Mweyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula.Picha na Freddy Maro-IKULU

Wednesday, 13 February 2013 03:15

Polisi waanza kuwafuatilia waliomtukana Spika

 

                                          Spika wa Bunge,Anne Makinda 

MWANANCHI
 

POLISI mkoani Dar es Salaam wametangaza kuwafuatilia, kuwasaka na kuwachukulia hatua wote waliotuma ujumbe wa matusi ama kupiga simu ya vitisho kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda. Viongozi wa Chadema walifanya mkutano wao mwishoni mwa wiki kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, jijini Dar es Salaam na kutoa namba za Spika wa Bunge ili mashabiki wamshinikize ajiuzulu. Pia viongozi hao walitoa namba za simu za Naibu Spika, Job Ndugai ili naye ashinikizwe ang’oke katika nafasi yake kwa madai ya kukandamiza upinzani bungeni. Chadema walidai kuwa

Tuesday, 12 February 2013 18:03

kamati ya tff yasimamisha kampeni

TanzaniaFootballFederation1 a03d5

Kamati ya Uchaguzi, kwa mamlaka iliyonayo kupitia Kanuni za Uchaguzi za TFF Ibara ya 3(1), 6(1) (g) na (l), 10(5), 11(6) inayosomeka pamoja na Ibara ya 14(1) na (2) na pia Ibara ya 26(5) na (6), imesitisha zoezi la kampeni za uchaguzi wa TFF na TPL Board lililokuwa lianze kesho tarehe 13/02/2013 hadi hapo itakapowatangazia, ili kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unakidhi kikamilifu matakwa ya Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF.

 

2. Tarehe za Uchaguzi Mkuu wa TFF na TPL Board zinabaki kama zilivyopangwa.

 

3. Taarifa hii inazingatia pia Ibara ya 2(4) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF inayoagiza uongozi uliopo madarakani kuendelea na kutekeleza majukumu ya Shirikisho hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.

 

Deogratias Lyatto

MWENYEKITI

KAMATI YA UCHAGUZI TFF

Tuesday, 12 February 2013 15:36

baraza la wafanyakazi ujenzi lazinduliwa

 Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akizindua kitabu cha Mwongozo wa Usanifu wa Barabara. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Saidi Amani na kushoto ni Eng. Joseph Nyamuhanga, Mkurugenzi wa Barabara katika Wizara ya Ujenzi.

 

Tuesday, 12 February 2013 15:18

prof muhongo atoa leseni ya madini chunya

pro 0634e

Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akikabidhi leseni ya uchimbaji madini kwa Bw. Roman Lyaruu kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Itewe wilaya ya Chunya. Mhe. Waziri alisisitiza wachimbaji wa madini kulipa kodi zote zinazotozwa na Mamlaka za Serikali ikiwemo mrabaha wa asilimia nne.

Tuesday, 12 February 2013 14:34

UCHAGUZI FRAT UPO PALEPALE FEB 14

 

 

 

TFF a1e7a

Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) unafanyika Februari 14 mwaka huu mjini Morogoro kama ulivyopangwa, tofauti na taarifa wanazopewa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho. Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya FRAT, Damas Ndumbaro, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa FRAT wanatakiwa kufika Morogoro keshokutwa (Februari 12 mwaka huu) . Pia

Tuesday, 12 February 2013 14:09

magereza wapata mafunzo juu ya jinsia

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima akimsalimia  Mwezeshaji wa Mafunzo ya Jinsia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Asina Omari (kulia) kabla ya kufungua mafunzo ya Jinsia awamu ya pili mjini Morogoro leo. Kushoto ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. Pereira aliwataka maafisa wa jeshi hilo wahakikishe msongamano ndani ya magereza nchini unapungua.

220px-Coat of arms of Tanzania.svg 883ff

 

                                   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Serikali  inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kuwa hivi karibuni kumezuka kundi la Watu wadanganyifu ambao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi waandamizi wa serikali na Taasisi nyeti ikiwemo Usalama wa Taifa kujipatia fedha  kwa madai ya kutumwa na viongozi hao. Watu hao wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kwa maofisa mbalimbali wa wizara, mashirika ya umma na Idara za Serikali zinazojitegemea kuomba pesa ili wawafanye mipango ya kupandishwa vyeo. Utapeli huo

Tuesday, 12 February 2013 13:03

JK.awatambulisha WajuMBe wa Kamati Kuu Dodoma

8E9U8863 a62b3

Mwenyekiti wa CCm Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM nje ya ukumbi wa White House,Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.

 

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi