We have 156 guests and no members online

mjengwablog

mjengwablog

Baadhi ya wachimbaji madini katika moja ya migodi huko DRC.

Picha kwa hisani ya AFP.

Taarifa za awali kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC zinasema Polisi wa kwenye eneo la Rubaya Masisi katika jimbo la Kivu kaskazini mwa DRC wanashutumiwa kuwafyatulia risasi na kuwauwa wachimbaji madini watatu katika mgodi wa Rubaya.

Image result for LAW

Mahakama nchini Pakistan imemhukumu mwanume mmoja adhabu ya kifo na kuwatia hatiani wengine 30 kuhusiana na tukio la kuchomwa kwa mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 23 aliyetuhumiwa isivyokweli kukashifu dini.

Thursday, 08 February 2018 05:17

TARATIBU ZILIZOWEKWA KUMUONDOA ZUMA MADARAKANI.

Image result for jacob zuma

Kiongozi wa chama tawala cha African National Congress (ANC) nchini Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amesema anazungumza moja kwa moja na Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma, kujadili masharti ya kujiuzulu na kuhakikisha mabadiliko katika uongozi wa taifa hilo.

Image result for joseph haule

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Nyasa kimedai kuwa mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Prof. Jay na mkewe wamezuiliwa kuwanona Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga katika Gereza la Ruanda ambako wamewekwa mahabusu.

Related image

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi, amesema hakuna mgongano mkubwa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar unaosababisha ongezeko la kero za Muungano.

Image may contain: 1 person, standing and outdoor

Na MAGGID MJENGWA.

Kuna kisa cha mwana wa gavana katika Misri ya kale. Mwana yule alitembea akijivunia cheo cha baba yake.akajawa kiburi kufikia siku moja kumdhalilisha mwalimu wa shule mtaani huku watu wazima na watoto wengine wakiangalia. Ndio, mwana yule alimchapa bakora ya matakoni mwalimu yule, tena hadharani. Mwalimu alifedheheshwa sana, maana hata kosa hakulijua. Mwalimu yule akafunga safari ndefu kwenda kuarifu jambo lile kwa mfalme wan chi. Huko akapokelewa, akaeleza yaliyomsibu.

media

Watu wasiojuliana wameripotiwa kujipenyeza katika hospitali maarufu katika kata ya Ndosho, mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na kuwachoma visu wagonjwa 12 wakiwa wodini.

Image result for MORGAN TSVANGIRAI IN HOSPITAL

Hali ya Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai inaelezwa kuwa mbaya zaidi mapo mpaka sasa yuko katika hospitali moja nchini Afrika Kusini. Taarifa zilizotolewa na familia yake kwa vyombo vya habari zinasema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 ambaye anatibiwa saratani ya matumbo anakabiliwa na upungufu wa uzani , kuchoka na mishipa yake ya damu kua membamba. Tsvangirai ambaye ndiye kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC nchini Zimbabwe anafahamika zaidi kwa harakati zake dhidi ya aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe , na amepigwa na kufungwa jela mara kadhaa.

Image result for JOHN TSHIBANGU

Kanali muasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, John Tshibangu, amefikishwa nchini humo na kuzuiliwa kusikojulikana nchini humo, baada ya kukamatwa nchini Tanzania. Awali serikali ya DRC ilithibitisha kumpokea Kanali John Tshibangu aliyekamatwa na vyombo vya usalama vya Tanzania juma moja lililopita baada ya kuonekana kwenye mkanda wa video akimpa siku 45 rais Joseph Kabila awe amejiuzulu au aipindue Serikali yake.

Image result for FEMALE GENITAL MUTILATION

Dunia hii leo inaadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji kwa wanawake FGM inayolenga kuimarisha kasi kuelekea kumaliza utamaduni huo unaochukuliwa kimataifa kama ukiukwaji wa haki za binaadamu kwa wasichana na wanawake. Zaidi wa wanawake na wasichana milioni 200 wanakisiwa kufanyiwa ukeketaji wa aina mbalimbali huku kiasi ya wasichana milioni 44 wenye umri wa miaka 14 na chini ya hapo wakiwa wamekeketwa.

Page 5 of 3154

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji