We have 158 guests and no members online

mjengwablog

mjengwablog

Image result for NDEGE ILIYOANGUKA ZANZIBARNa Muungwana blog.

Ajali hiyo ilitokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume majira ya saa 7:00 mchana, wakati ndege hiyo ikijaribu kuruka, hitilafu ya mfumo wa umeme imetajwa kuwa chanzo kikuu cha ajali ya ndege ambayo ilisababisha vifo vya watu wawili juzi visiwani Zanzibar. Hata hivyo mbali na sababu hiyo, Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) cha Dar es Salaam, Dk. Bwire Rufunjo, almesema uchunguzi zaidi wa chanzo cha ajali hiyo unaendelea hata hivyo.

Image result for Sebastien Yebo

Padri Sebastien Yebo wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Robert katika eneo la N'sele jijini Kinshasa- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ameachiliwa huru jumapili hii. Padri huyo alitekwa siku ya jana Jumamosi na Polisi baada ya kuongoza misa ya asubuhi katika Kanisa hilo. Padri Yebo amezungumza na shirika la habari la RFI na kuthibitisha kuachiliwa kwake, lakini hakueleza hali ilivyokuwa baada ya kukamatwa.

Image result for Danladi Umar

Nchini Nigeria Jaji mmoja wa ngazi ya juu anayeshughulikia kesi za tuhuma za rushwa ameshatakiwa kwa kosa la rushwa hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa nyaraka za kimahakama nchini humo. Jaji huyo Danladi Umar anatuhumiwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini humo ya EFCC kwa kuomba rushwa kutoka kwa mtuhumiwa ya naira milioni kumi ambayo ni sawa na dola 27,800 ili aweze kutoa upendeleo kwa mtuhumiwa huyo hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa nyaraka za kimahakama ambazo pia zimeshuhudiwa na shirika la habari la AFP.

Image result for zitto kabwe msibani kwa kingunge

Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe amevitaka vyama vya Chadema na CCM kusimamisha kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani kwa siku tatu kama sehemu ya kuomboleza kifo cha mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru. Akiwa kwenye msiba wa mwanasiasa huyo Kijitonyama, Zito amesema Kingunge alisaidia kuimarisha chama cha mapinduzi CCM na baadaye CHADEMA, hivyo sio busara vyama hivyo kuendelea na kampeni

Image result for joachim wangabo

Joachim Wangabo Mkuu wa mkoa wa Rukwa, ameagiza mkuu wa shule ya sekondari Muhama manispaa ya Sumbawanga mkoani humo kuchukuliwa hatua za kisheria kwa tuhuma ya kuwatoza wanafunzi michango ya Sh5,000 kama gharama ya kuwapatiwa fomu za maelezo ya kujiunga na shule hiyo. Wangabo ametoa agizo hilo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kata ya Malangali baada ya baadhi ya wananchi kulalamikia jambo hilo, kwamba wazazi waemekuwa wakichangishwa pesa hiyo ili kugharamia fomuza kujiunga.

Image result for catholic church in drc

Chanzo, DW.

Jeshi la polisi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jumamosi limetajwa kumteka nyara padri mmoja baada ya misa mjini Kinshasa kumalizika. Hayo yameelezwa na walioshuhudia wakati nchi hiyo ikiwa katika wasiwasi na mvutano mkubwa baina ya kanisa na serikali kuhusiana na hatua ya rais Kabila ya kukataa kuondoka madarakani. Mtawa mmoja alieyeshuhudia tukio hilo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa Padri Sebastien alichukuliwa mateka na polisi muda mfupi baada ya kumalizika misa katika kanisa la parokia ya Mtakatifu Robert,

Tokeo la picha la MWIGULU NCHEMBA AKIWA TABORA
 
Watendaji wanaosimamia usajili wa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa wametakiwa kuwa makini katika zoezi hilo. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba wqakati akizungumza katika uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho hivyo kwa wakazi wa Tabora, amesema umakini huo utasaidia vitambulisho hivyo kutotolewa kwa watu wasiostahili.

Tokeo la picha la KENYA MEDIA

Tokeo la picha la KENYA MEDIA

Umoja wa mataifa UN umeongeza agizo jipya dhidi ya hatua iliyochukuliwa na serikali ya Kenya kwa vituo vitatu vya Televisheni. Katika agizo hilo Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya Kenya kuheshimu tamko la mahakama lililoagiza kuvifungulia matangazo vituo vya KTN News, Citizen TV na NTV. Shirika la umoja wa mataifa la haki za binadamu liliwasilisha malalamishi yake kwa umoja wa mataifa na Umoja wa Ulaya EU, baada ya hatua ya serikali ya Kenya kuvifungia mitambo ya matangazo vituo hivyo vya runinga, na kushinikiza serikali ya Kenya kuachana na hatua hiyo inayominya uhuru wa vyombo vya habari.

Saturday, 03 February 2018 05:15

WAHAMIAJI 90 WAHOFIWA KUFA MAJI LIBYA.

Tokeo la picha la Ninety feared dead after shipwreck off Libya coast
Picha inayohusianaShirika la uhamiaji la kimataifa (IOM) limeripoti takriban wahamiaji 90 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama katika pwani ya Libya. Baadhi ya wahamiaji walionusurika wamesema wengi wa wahamiaji hao walikuwa ni raia kutoka Pakistan. Katika taarifa za awali zilizoripotiwa na shirika la habari la Ufaransa RFI, zinasema watu watatu tu ndio wanaoaminika kunusurika. Katika kipindi cha miaka minne iliyopita Wahamiaji haramu zaidi ya 600,000 walifanya safari zinazoaminika kuwa za hatari kati ya Libya na Italia. Katika kipindi hicho, wahamiaji 6,624 waliingia Ulaya kupitia bahari ya Mediterranean, ambapo kwa mujibu wa shirika la uhamiaji la kimataifa, IOM, wengine 246 walikufa maji wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean.
Friday, 02 February 2018 14:52

TAKUKURU YAWANASA WANNE TEMEKE.

Tokeo la picha la takukuru

Chanzo; Mwananchi.

Emanuel Kobelo Ofisa mtendaji wa kata ya Jangwani, Joseph Chilumba ni ofisa mstaafu wa jeshi la magereza, Ally Ally mfanyabiashara wa kampuni ya Equlmalk pamoja na Doroth Magige wametiwa mbaroni na TAKUKURU kwa kosa la kuomba rushwa. Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Temeke Pilly Mwakasege amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kwa kuwekewa mtego tarehe 30 January mwaka huu, baada ya kumuomba rushwa ya shilingi milioni 3 ili wasimchukulie hatua Ally Ally mfanyabiashara waliyemtuhumu kushirikiana na raia wa kigeni katika kufany abiashara ya madini ya dhahabu na almasi.

Page 7 of 3154

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji