We have 158 guests and no members online

mjengwablog

mjengwablog

Tokeo la picha la Etienne Tshisekedi

 

Ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kifo cha aliyekua mpinzani mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Etienne Tshisekedi wa Mulumba, mwili wake unaelezwa kuwa bado haujarejeshwa nchini humo kwa minajili ya kuzikwa.Etienne Tshisekedi alifariki dunia Februari 1, 2017 nchini katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels. Kutokana na kukosekana kwa makubaliano kati ya chama cha UDPS na serikali mjini Kinshasa, mwili wa Tshisekedi bado umesalia katika chumba cha kuhifadhi maiti mjini Brussels.

Tokeo la picha la bobo haram attack

Takribani watu wanne wamepoteza maisha katika shambulio la kujitoa muhanga lililotokea kwenye kambi ya wakimbizi mjini Maiduguri Kaskazini mashariki mwa Nigeria ambapo kundi la Boko Haram linaaminika kuhusika na shambulio hilo.

Benki ya Exim Tanzania imetoa msaada wa vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya, wodi ya wazazi Meta, ikiwa ni sehemu ya sherehe ya miaka 20 ya kutoa huduma iliyoanza kuadhimishwa mwezi Agosti mwaka jana.

Thursday, 01 February 2018 13:05

TATIZO LA MAJI LINDI MJINI KUBAKI HISTORIA

Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo amefanya ziara kutembelea mradi wa maji wa Ng’apa Mkoani Lindi wenye thamani ya Euro milioni 11.7 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali.

 

Tokeo la picha la kenyan journalistsChanzo, DW.

Wanahabari watatu wa Kenya walilazimika kukesha katika chumba cha habari kwa kuhofia kukamatwa na polisi waliokuwa wameweka kambi nje ya majengo ya shirika la habari la habari la Nation. Mawakili wa wanahabari hao wamewasilisha maombi mahakamani ya kutaka hakikisho la uhuru wa wanahabari hao.

Tokeo la picha la prof mbarawa TTCL

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ametoa tamko rasmi la kuibadilisha  kampuni ya mawasiliano TTCL kutoka kampuni ya mawasiliano na sasa litakuwa Shirika la Mawasiliano la umma.

Tokeo la picha la Okiya Omtatah

Mwanaharakati nchini Kenya Okiya Omtatah ametinga mahakamani kupata mwafaka kisheria kuhusu kufungwa kwa vituo vitatu vya runginga nchini humo jambo ambalo ameliita ni kinyume cha katiba ya nchi. Katika madai yake ambayo yanatakiwa kusikilizwa leo Februari mosi, Bw. Omtatah amesema uamuzi wake wa kwenda mahakamani ni kutokana na uamuzi wa serikali kuvifungia vituo vya NTV, Citizen na  KTN News na kwamba uamuzi huo unakiuka kifungu namba 33 na 34 cha katiba ya nchi.

Thursday, 01 February 2018 05:10

MSIMAMO LIGI KUU EPL BAADA YA MECHI ZA JANA.

Tokeo la picha la epl

Hapo jana January 31, 2018 ilishuhudiwa michezo kadhaa katika ligi ya Uingereza (EPL)

Mechi kubwa ilikuwa ni kati ya Tottenham dhidi ya Manchester United mchezo uliomalizika kwa Tottenham kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Michezo mingine ilikuwa kama ifuatavyo;

                       Chelsea 0-3 Bournemouth

                       Everton 2-1 Leicester City

                       Southampton 1-1 Brighton and Hove Albion

                      Manchester City 3-0 West Bromwich Albion

                       Stoke City 0-0 Watford

Baada ya michezo hiyo huu msimamo wa ligi kuu uko hivi;

 

Tokeo la picha la nkurunziza

Wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni na wale waliosalia nchini Burundi wamekubaliana kuachana na mpango wa kuanzisha vita nchini humo kwa lengo la kumtimua rais Pierre Nkurunziza. Wanasiasa hao wameafikiana masuala muhimu hasa kuungana dhidi ya kura ya maoni yenye lengo la kufanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo iliyopangwa kufanyika mnamo mwezi Mei 2018 na hivyo kuruhusu Rais Pierre Nkurunziza kusalia madarakani hadi mwaka 2034.

Page 9 of 3154

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji