habari

JPM Afanya Uzinduzi Wa Mradi Wa Usimikaji Wa Rada

on

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amezindua mradi wa usimikaji wa rada nne za kuongozea ndege zitakazofungwa  katika viwanja vya ndege vya Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro na Mbeya.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo rais Magufuli amesema kwa miaka mingi Tanzania ilikuwa inatumia rada moja tu kuongozea ndege iliyokuwa ikihudumia asilimia 25 pekee ya anga lote la Tanzania na hivyo kupoteza shilingi bilioni 1.2 kwa kukasimu anga lake kwa nchi jirani

Amesema rada hizo nne ambazo ununuzi na ujenzi wake utagharimu bilioni 67.3 zitasaidia kuziona na kuongoza ndege zote zinazopita kwenye anga ya Tanzania na hivyo kuongeza usalama pamoja na kukuza mapato ya serikali

Rais Magufuli amemwagiza Waziri wa Ujenzi pamoja na Mamlaka ya usimamizi wa viwanja vya ndege kusimamia ujenzi wa mradi huo ukamilike kwa wakati huku pia akiagiza mkandarasi anayenga jengo la kuongozea ndege katika uwanja wa Mwanza kukamilisha ujenzi haraka

Wakati huo huo Rais Magufuli ameipokea ndege ya tatu aina ya Bombadier iliyonunuliwa mwaka jana na kushikiliwa nchini Canada na kuwataka watanzania wajivunie maendeleo kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *