habari

JPM “Inabidi Tujikinge Na Kuchukua Tahadhari Zote Kwa Gonjwa Hili.”

on

Rais John Pombe Magufuli amewataka wakazi wa mikoa ya Njombe na Iringa kuchukua tahadhari juu ya gonjwa la Ukimwi sababu mikoa hiyo ndio inayoongoza nchini. Rais amesema hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospital ya Kilolo.

“Mkoa wa Iringa na Njombe ina maambukizi mengi ya UKIMWI, Iringa una 11.2% na Njombe ni 11.6%. Inawezekana sababu ya msingi ni baridi lakini sina uhakika. Ni lazima tuwajibike katika kujikinga na UKIMWI,” amesema Rais Magufuli.

“Kwahiyo Iringa ni ya pili Njombe ni ya kwanza kwa maambukizi ya Ukimwi nilipofika hapa Kilolo inaonekana shida kubwa hapa ni baridi na kwasababu inaletwa na Mwenyezi Mungu inabidi tujikinge na kuchukua tahadhari zote kwa gonjwa hili.”

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *