habari

Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa TRA Kupandishwa Cheo.

on

Rais John Magufuli amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kumpandisha cheo mara moja Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa Mamlaka ya Mapatao Tanzania (TRA) bandari ya Dar es Salaam, Ben Usaje (kwenye picha, kulia) na kuwa Kamishna kamili.

Rais ametoa agizo hilo leo Jumanne Mei 15, 2018 wakati akizungumza viongozi mbalimbali wa TRA, Bandari, TBS na ulinzi alipofanya ziara ya kushtukiza kukagua matanki yenye mafuta yaliyodaiwa kuwa ni ghafi (crude oil).

“Nawapongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kazi nzuri mnayoifanya, Waziri wa Fedha, mpeni tu huyu ukamishna kamili kwa sababu amesimamia haki kwa maslahi mapana ya nchi yetu, najua wapo wanaomchukia sana, wengine ni wafanyabiashara lakini waache wakuchukie Mungu anakupenda na Watanzania tutaendelea kukupenda. Kwa hiyo, waziri mka-confirm. Katibu Mkuu mkazungumze wote, ikiwezekana mumpandishe cheo ndani ya wiki hii msimcheleweshe”, amesema Rais Magufuli.

Uamuzi huo wa Rais Magufuli umekuja baada ya kumuuliza swali Kaimu Kamishna kuwa anafanya kazi gani TRA na ndipo alipotoa amri hiyo ya kupandishwa cheo haraka kutokana na kuwa ameweza kusimamia haki bila kupindisha.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *