habari

Katibu mkuu Chadema matatani baada ya kushindwa kufika Mahakamani leo

on

 

Mwandishi wetu Dar Es Salaam.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salam imemtakaka katibu mkuu wa  Chadema, Dk Vicent Mashinji kufika mahakamani hapo na kuileza mahakama hio zilizopelekea yeye ashindwe kuhudhuria  kesi yake iliyopo mahakamani hapo.

Uamuzi huo umefikiwa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, baada ya upande wa mashtaka kupinga maelezo ya barua yaliyotolewa  na upande wa utetezi kuwa mshtakiwa yupo katika katika kesi nyingine iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea.

Kufuatia kukosekana mahakamani hapo kwa Dk Mashinji hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi kesho ikitarajiwa  kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka,

Awali, kabla ya Mahakama hiyo kutoa uamuzi huo, jopo la mawaliki watatu wa Serikali, likiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, liliieleza  mahakama hiyo kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi na upande wa mashtaka na wapo tayari.

Nchimbi baada ya kueleza hayo, kiongozi wa jopo la mawakili wanne wa utetezi, Profesa Abdallah Safari, alidai kuwa mshtakiwa wa sita katika kesi hiyo Dk Vicent Mashinji amewasilisha barua mahakamaji hapo kuwa yupo kwenye kesi yake nyingine ya jinai namba 9/2017 iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea.

Profesa Safari alidai mteja wake ameshindwa kufika mahakama ya Kisutu kutokana na kesi inayomkabili  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea, kuwa ipo katika hatua ya utetezi na kwamba anatakiwa kujitetea kwa siku mbili mfululizo kuanzia April 15 na 16, 2019

Hoja ya kwanza, walidia kuwa  taarifa zilizowasilishwa na upande wa utetezi hazijajitosheleza, kigezo alichotumia mshtakiwa kwenda Mahakama ya Songea wakati akijua kuwa anakesi Mahakama ya Kisutu, huku  hoja ya pili ni kibali kilichotolewa na mshtakiwa cha kuruhusu mahakama kuendelea na shauri hilo, bila ya mshtakiwa kuwepo mahakamani hapo.

” Taarifa zilizowasilishwa na upande wa utetezi hazijitoshelezi kwa sababu  mshtakiwa alikuwepo wakati  mahakama hii inapanga tarehe ya kuanza kusikiliza shauri hili, hivyo alipaswa kutuambia kuwa April 15 na 16, mwaka huu, atakuwa na kesi nyingine ili mahakama hii ipange terehe nyingine ambayo haitaingiliana na ile ya Songea” alidai Nchimbi.

Wakili Nchimbi alidai  kuwa mshtakiwa anatambua kuwa anakesi mahakama ya Kisutu na alipaswa kutoa taarifa mapema, hivyo wanatarajia kupata maelezo ya kina  kutoka kwake ametumia kigezo gani cha kwenda ya Hakimu mkazi Songea.

Wakili Nchimbi alifafanua kuwa utaratibu wa kisheri kwa mujibu wa Kifungu namba  196 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai( CPA) sura ya 20 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002, kinaeleza wazi kuwa ushahidi wowote unaotolewa mahakamani ni lazima utolewe mbele ya mshtakiwa au washtakiwa wote wanaohusika katika shauri hilo na kama mshtakiwa ni mgonjwa basi anatakiwa kuwa na uwakikishi wa wakili na kuwasilisha  kibali ambacho kinaridhia kesi yake  kuendelea  bila ya yeye kuwepo.

Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja za pande zote, alisema kuwa kesi hiyo itaendelea kesho( April 17,2019) na Dk Mashinji anatakiwa kuwepo mahakamani hapo.

Mbali na Dk Mashinji, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe; Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko;   Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa; Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu;  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Kawe,  Halima Mdee, Mbunge wa Tarime vijijini, John Heche na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na makosa 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, February 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *