habari

Kesi Ya Viongozi Wa Chadema, Maamuazi Ya Dhamana Kutolewa.

on

Kesi ya Viongozi wa CHADEMA inatarajiwa kutajwa leo chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye anatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu dhamana ya washtakiwa hao. Katika kesi hiyo, Viongozi waandamizi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefikishwa mahakamani leo saa 2 asubuhi katika Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa dhamana yao huku wakisindikizwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati kuu CHADEMA.

Baadhi ya Viongozi wengine wa CHADEMA wakiwa mahakamani ili kuwasindikiza viongozi wenzao wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Profesa Abdallah Safari na Wabunge wengine.

Baadhi ya wabunge wa Chadema, wafuasi wa chama hicho na wananchi wengine waliofika mahakamani kufuatilia kesi hiyo.

Umati wa watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwa wamekusanyika nje ya mahakama.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *