habari

Kiongozi Wa Dini Auwawa Kwa Kupigwa Risasi Na Waasi.

on

Taarifa zilizotolewa na vyombo vya usalama, zinasema Kasisi mmoja wa kanisa katoliki ameuawa kwa kupigwa risasi na waasi wa kundi la Mai Mai Nyatura Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo.

Vyanzo hivyo vimeongeza kuwa Padri Étienne Nsengiyumva aliuawa wakati wa sherehe za ibada ya ubatizo wa wakristo wapya na wanandoa wapya. Mashahidi wanasema mtu mwenye silaha aliingia kanisani na kumpiga risasi kasisi huyo.

Hii si mara ya kwanza kutokea kwa vitendo viovu dhidi ya viongozi wa kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mauaji na visa vya utekaji nyara dhidi ya viongozi wa kanisa Katoliki vinaendelea kushuhudiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hasa mashariki mwa nchi hiyo.

 

Katika kipindi kisichozidi wiki mbili Padri Havugimana Ngango Célestin alithibitishwa kutekwa nyara na waasi wasiojulikana katika maeneo ya Kihondo wilayani Ruchuru, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Padri Ngango alitekwa nyara na waasi wasio julikana akiwa kwenye gari lake kwenye barabara inayoelekea Kihondo katika eneo la Nyarukwangara ambako alisherehekea pasaka.

Mwanzoni mwa mwaka huu Padri mmoja alitekwa nyara na kundi la waasi ambalo halikujulikana. Wanaharakati wa haki za binadamu wanaomba serikali ya DRC kufanya kazi yake ya kulinda raia ipasavyo.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *