habari

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Chalaani tukio la trafiki watatu kumshambulia dereva

on

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimelaani tukio la askari wa Jeshi la Polisi kutumia nguvu kupita kiasi kupambana na raia.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Januari 14, 2019 na kituo hicho na kusainiwa na mkurugenzi mtendaji wake, Anna Henga imeeleza kuwa kufanya hivyo ni kinyume na  sheria ya kanuni ya adhabu sura 16, sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 na sheria ya jeshi la polisi na huduma saidizi sura ya 322.

Tamko hilo limekuja kufuatia kusambaa kwa video inayowaonyesha askari watatu wakitumia nguvu kupita kiasi wakati wa kumkata mtuhumiwa katika mji wa Tunduma, mkoani Songwe.

Katika taarifa hiyo LHRC imelitaka jeshi la polisi kuzingatia haki katika utekelezaji wa majukumu yake huku likilinda uhai wa raia na mali zake.

Sanjari na hilo kituo hicho kimewaasa wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi pale wanapotimiza wajibu wao ikiwemo kukamata, kuhoji, kupekua ili kuepusha ulazima wa matumizi ya nguvu kubwa dhidi ya raia.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *