michezo

Kocha Wa Timu Ya Taifa Ya Japan Atimuliwa.

on

Japan imemfukuza kocha wake mkuu wa kandanda Vahid Halilhodzic. Katika uamuzi huo wa ghafla, Vahid anakuwa mwalimu wa tano wa Timu ya taifa ambayo ni mwakilishi wa Asia katika Kombe la dunia 2018, kuachishwa kazi katika kipindi cha miezi tisa iliopita.

Aidha inaelezwa kuwa Iran ndiyo nchi pekee ambayo kocha wa timu ya taifa Carlos Queiroz, anayeendelea na kazi yake tangu 2011 huku mataifa ya Japan, Saudi Arabia na Australia, yote yakiwa na makocha wapya watakaoziongoza timu zao katika fainali za kombe la dunia mwezi Juni nchini Urusi.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *