habari

Korea Kusini Kuondoa Vipaza Sauti Vinavyotangaza Propaganda.

on

Korea Kusini imesema itaondoa vipaza sauti ambavyo mara kwa mara hutangaza propaganda zinazoilenga Korea Kaskazini hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya nchi hiyo katika taarifa yake leo Jumanne.

Korea Kusini ilikuwa tayari imezima kipaza sauti chake kabla ya mkutano wa kilele kati ya nchi hizo mbili hatua iliyofuatiwa na Korea Kaskazini ambayo pia ilisimamisha matangazo yake ya aina hiyo. Uamuzi huo ni moja ya hatua za awali za kuboresha mahusiano kati ya pande hizo mbili baada ya rais wa Korea Kusini Moon Jae In kukutana Ijumaa iliyopita na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *