habari

Kuahirishwa Kwa Zoezi La Ajira Za Watumishi Wa Muda Kwa Ajili Ya Uboreshaji Wa Daftari La Kudumu La Wapiga Kura

on

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa tarehe 30 Mei, 2019 iliwatangazia nafasi za kazi za muda kupitia tovuti yake ya www.nec.go.tz na kuwaalika watanzania wenye sifa zilizo ainishwa kwenye tangazo hilo kuomba nafasi hizo za kazi.
Hivyo, Tume inapenda kuwataarifu wananchi wote ya kwamba mchakato wa ajira za muda kwa ajili ya zoezi hilo umeahirishwa hadi hapo itakapotangazwa tena.
Aidha, Tume inapenda kutoa shukrani zake kwa wale wote walioleta maombi yao ya kazi na inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Dkt. Athumani Kihamia
MKURUGENZI WA UCHAGUZI

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *