michezo

Kuelekea Kufungwa Dirisha La Usajili Ulaya Linavitesa Vilabu Vya EPL

on

Wakati dirisha kubwa la usajili lilipofungwa mwaka jana, moja kati ya mambo yaliyozungumzwa sana ni jinsi ambavyo Leicester City walivyoshindwa kumsajili Adriein Silva kutoka Ureno wakichelewa kwa sekunde 14 kuwasilisha nyaraka muhimu hali iliyowalazimu kusubiri mpaka mwezi January uliofuatia wakati dirisha dogo lilipokuwa wazi.

Kila mtu anakumbuka kilichowahi kuwakuta Manchester United wakati walipojaribu kumsajili Ander Herrera kutoka Athletic Bilbao au ile story ya mashine ya fax iliyofelisha deal la David De Gea kwenda Madrid na Keylor Navas kwenda Manchester United.

Matukio yote haya yanaashiria ugumu uliuopo kwenye biashara ya wachezaji kutoka timu moja kwenda nyingine na baada ya baadhi ya makocha kulalamikia wachezaji wao  kukosa umakini kwa sababu ya ligi kuendelea huku dirisha la usajili likiwa wazi.

Timu za ligi ya England kwa wingi wa timu 15 kwa 5 zilipiga kura na kuamua kuwa dirisha la usajili kwenye ligi ya Malkia litafungwa mapema kuliko sehemu nyingine kitu ambacho timu hizi 15 zilizopigia kura maamuzi haya, hazikuwa na uwezekano mkubwa wa timu za maeneo mengine barani Ulaya kusajili wachezaji huku timu zao zikishindwa kusajili wachezaji wa kuziba mapengo.

Waliwaza nini viongozi kama Daniel Levy ambaye hadi sasa timu yake ipo hatarini kuwapoteza Danny Rose na Toby Alderweireld lakini wana siku tatu tu za kusajili wabadala huku pia wakifahamu jinsi ambavyo mshambuliaji Fernando Llorente anavyotaka kuihama timu hiyo lakini wanampata nani wa kumnunua huku dirisha linafungwa ndani ya saa pungufu ya 72?

Daniel Levy ni miongoni mwa watu waliounga mkono dirisha la usajili EPL kufungwa mapema. Manchester United waliweka wazi azma ya kumtaka Toby tangu mwezi May wakijua wazi Spurs watalazimika kumuuza kwani anataka kuondoka na pia anakipengele kwenye mkataba wake kinachoonesha kuwa asipouzwa msimu huu anaweza kuuzwa msimu ujao kwa nusu ya kiasi anachoweza kuuzwa leo.

Levy akijua kuwa United watalipa zaidi, alikataa offer ya kwanza ya United na miezi mitatu baadaye anakaribia kukubali offer ile ile ya United kwa kiwango kilekile huku akiwa hajasajili mbadala.

Manchester United ambao hawakuunga mkono wazo hili, wapo hatarini kumpoteza Paul Pogba ambaye vyombo vya habari kama Mundo Deportivo gazeti la kila siku huko Hispania limeripoti kuwa, wakala Mino Raiola ametua Manchester United akiwa na lengo la kulazimisha mteja wake kuondoka United akihitajiwa na Juventus ya Italia na Barcelona ya Hispania. Haya yote yakitimia, Manchester United wanaweza kupata fedha nyingi lakini hawatapata muda wa kusajili mbadala.

Vipi kuhusu Leicester ambao wanakaribia kumpoteza nyota wa England Harry Maguire kwa ongezeko la zaidi ya 50% kwenda Manchester United? Lakini watalazimika kumchukua mchezaji wa United ambaye hawakuwa na mpango wa kumsajili wala hajakutana na wenzie kutengeneza uelewano kabla ya kucheza pamoja.

Je, Chelsea ambao zikiwa zimebaki siku chache lakini bado hawajua kama watambakiza golikipa Thibaut Courtois? Ambaye ripoti zinasema ameshatuma maombi rasmi ya kuuzwa.

Ligi ya England inatarajia kuanza Ijumaa ya August 10, 2018 huku dirisha la usajili nchini humo likiwa limefungwa saa 24 kabla ya hapo lakini bado litaendelea kwenye mataifa mengine ya Ulaya ambayo hayatakuwa na kitu cha kuwazuia kutokwenda England kununua wachezaji.

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *