habari

Kukosekana Mashine Ya X-ray Kwasababisha Usumbufu Hospitali Ya Wilaya Mkuranga.

on

Hospitali ya wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani inakabiliwa na ukosefu wa mashine ya x-ray hali inayolazimu uongozi wa hospitali na ndugu kupeleka wagonjwa wao katika hospitali ya taifa Muhimbili na Mloganzila ili kupata vipimo

Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Steven Mwandambo amesema hospitali hiyo haina mashine ya x-ray tangu ianzishwe na wamekuwa wakiwasafirisha wagonjwa hadi Muhimbili kupata vipimo vya X-ray

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Mshamu Munde amesema licha ya kuwepo kwa chumba cha x-ray na wataalamu, bado hawajapata mashine hiyo na wanaendelea na juhudi za kuzungumza na wadau ili kupatiwa mashine

Amesema juhudi hizo za kupata mashine ya x-ray zinahusisha wadau ikiwemo wizara ya afya na mbunge wa jimbo la Mkuranga na kwamba kwa sasa wanawasiliana na ubalozi wa China ambao umeonesha nia ya kusaidia.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *