habari

Kwa Mara Ya Kwanza Mugabe Afunguka.

on

Robert Mugabe aliyekuwa Rais wa Zimbabwe amevunja ukimya kwa mara ya kwanza tangu aondolewe Madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi.

Akiongea na televisheni ya Afrika kusini ya SABC Mugabe amesema kuwa Rais wa sasa Emerson Mnangagwa asingeweza kuingia madarakani bila kutumika kwa jeshi.

Akiwa katika nyumba yake ya kifahari mjini Harare Mugabe amekemea mbinu zilizotumika kumuondoa madarakani na kwamba alikua tayari kufanya mazungumzo na Rais wa sasa Emerson mnangagwa na angehakikisha mabadiliko ya madaraka ya uhalali na si yale ya kulazimishwa ili kulinda katiba yao. Amesema kuwa hakudhani kama angepoteza imani yake kwa Mnangagwa kwani yeye ndie alimsaidia kuingia serikalini.

”Siamini kama yeye Mnangagwa angeweza kuniondoa madaraki , nimemuingiza serikalini, nimemsaidia alipokua jela anataka kunyongwa, sikuwaza kabisa kama siku moja yeye ndio atakua mtu wa kunitoa madarakani”

Aidha Mugabe ameogeza kuwa madaraka ya sasa yameingia kwa njia zisizo halali. ”Lazima tufute aibu hii, ambayo tumejiletea wenyewe, hatuistahili, hatuistahili, hatuistahili , tafadhali hatuistahili kabisa.Tunatakiwa kuwa nchi inayoheshimu katiba, ndio tunaweza kuwa na mapungufu hapa na pale lakini bado lazima tuheshimu sheria.”

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, baadhi ya wazimbabwe wanashangazwa na mkongwe huyo wa miaka 94, na wengine wanaamini kuwa amepoteza uhalisia kabisa baada ya kuongoza kwa miaka 38, wakati wake sasa umekwisha.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *