simulizi

Kwanini Mkulima Mwamwindi Alimpiga Risasi RC Dr Kleruu?

on

Ndugu zangu,

Kwa mujibu wa ushahidi wa mahakamani. ( 212. Saidi Mwamwindi v. R. Crim. Sass. 37-Iringa-72, 2/10/72. – Jaji Onyiuke)

Mkulima Said Mwamwindi anakabiliwa na shtaka la kumuua kwa kumpiga risasi Mkuu wa Mkoa, Dr Wilbert Kleruu.

Mahakama inaelezwa, kuwa Said Mwamwindi alianza kwa kufanya kazi ya udereva hadi alipoamua kuacha kazi hiyo mwaka 1954 na kujihusisha na kilimo.

Alihamia kijijini Mkungugu na familia yake na kupewa kwa njia za kimila, eneo la kilimo.

Mahakama ilielezwa na mashahidi, Mwenyekiti na Makamu mwenyeki wa Kamati ya Uongozi wa Kijiji cha Mkungugu, namna kijiji kilivyoshughulikia na suala la mgawo wa maeneo ya kilimo ambayo yaliingizwa kwenye mfumo wa Ujamaa.

Kwamba mfumo wa Ujamaa haukupiga marufuku ya watu binafsi kumiliki mashamba.

Kwa vile Kijiji cha Mkungugu kiko kwenye barabara ya Iringa- Dodoma. Wanakijiji waliamua, kuwa upande wa kushoto wa barabara uwe ni kwa ajili ya mashamba ya Ujamaa.

Mkulima Said Mwamwindi mashamba yake yalikuwa pande zote mbili za barabara.

Mahakama inaelezwa matukio ya siku moja kabla ya mauaji. Aliyekuwa Bwana Shamba wa Tarafa ya Isimani yenye kuhusisha vijiji vya Ndolela, Tarafani, Igula na baadade Mkungugu, kuwa msimu wa kupanda mahindi ulikuwa unaendelea.

RC Dr Kleruu alikuwa kwenye kuhimiza Vijiji vya Ujamaa kulima mashamba yao ya Ujamaa na kuwahi kupanda mbegu za mahindi kabla ya msimu kumalizika.

Katika kuifanya kazi hiyo, RC Dr Kleruu alikwenda kutoka kijiji kimoja hadi kingine kuhimiza hilo, na wakati mwingine aliingia mwenyewe shambani na kushika jembe kusaidia kazi za kilimo.

Shahidi, Bwana Shamba wa Isimani, aliendelea kuieleza Mahakama, kuwa , Jumamosi asubuhi, Desemba 24, 1971, RC Dr Kleruu alifika Kijiji cha Ujamaa Tarafani, akaenda kwenye eneo la mashamba ya Ujamaa na kuanza kwa kukagua matrekta ya kilimo.

Baada ya hapo, RC Dr. Kleruu na Bwana Shamba waliondoka kwa pamoja kuelekea Kijiji cha Igula kukagua maendeleo ya kilimo cha mashamba ya Ujamaa.

Kutoka hapo wakaelekea Kijiji cha Ndolela. Walifika mchana. Mvua kubwa ilinyesha na kukatisha shughuli za kilimo. RC Dr Kleruu akaitisha mkutano na kuwauliza wanakijiji kama walikuwa tayari kuendelea na kazi za kilimo siku ya pili yake, ambayo ilikuwa ni siku ya Krismasi.

Wanakijiji walikubali na RC Dr Kleruu akaahidi kurudi tena kuwasaidia na kazi zao za kilimo, siku ya pili yake.

Turudi tena kwenye siku ya tukio la mauaji;

Mkulima Mwamwindi anachukua bunduki yake yenye midomo miwili. Anaijaza risasi na kutoka nje.

Anamwona RC Dr Kleruu amesimama mbele yake. Anaishusha bunduki yake usawa wa RC Dr Kleruu.

Anavyatua risasi mbili kwa kutumia kidole cha tatu cha kati. Risasi mbili mfululizo zinampiga RC Dr Keruu aliyesimama umbali wa futi nane kutoka kwenye baraza ya nyumba ya Mkulima Said Mwamwindi.

Kabla ya kufahamu kilichotokea baada ya hapa, Mahakama inaelezwa juu ya matukio mawili; tukio la shambani na la makaburini.

Itaendelea….

Maggid

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *