siasa

Licha Ya Kujiuzulu Kwa Waziri Mkuu Wa Jordan, Maandamano Yaendelea.

on

Maandamano ya kuipinga serikali yameanza tena nchini Jordan licha ya kujiuzulu kwa waziri mkuu wa nchi hiyo ambaye aliongoza hatua za kubana matumizi. Maelfu kadhaa ya Wajordan waliandamana kuelekea ofisi ya waziri mkuu anayeondoka madarakani Hani Mulki usiku hadi mapema leo alfajiri, wakidai serikali iondoe kabisa pendekezo la kuongeza kodi, ambayo wakosoaji wanasema inawalenga zaidi masikini na watu wa tabaka la kati.

Polisi wa kuzuwia ghasia walipambana na baadhi ya waandamanaji, wakijaribu kuwazuwia kuingia katika jengo la ofisi ya waziri mkuu, lakini maandamano hayo ambayo yameendelea kwa siku tano kwa kiasi kikubwa yalikuwa ya amani. Mulki alijiuzulu jana, wakati mfalme wa Jordan Abdullah II akijaribu kuingilia kati katika maandamano hayo makubwa kuwahi kutokea katika nchi hiyo ya kifalme kwa miaka kadhaa.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *