michezo

Liverpool Yatinga Finali ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

on

Roma imepata ushindi wa goli 4-2  dhidi ya Liverpool nakufanya matokeo kuwa jumla ya goli 6-7 ambayo yanaipeleka moja kwa moja timu ya Liverpool katika final ya mashindano hayo.

Liverpool ya Uingereza sasa itavaana vikali na Real madrid ya Hispania ambayo ni mabingwa mara mbili mfululizo katika michuano hiyo.

Fainali hiyo itafanyika tarehe 26 ya  mwezi huu katika uwanja wa NSC Olimpiyskiy  mjini Kiev, nchini Ukraine.

Mtanange huu utakuwa mgumu kati ya timu zote mbili kwa kiwango walichokionesha katika hatua ya nusu fainal ambayo Real madrid iliifunga timu ya Bayern ya Ujerumani na Liverpool kuifunga timu ya Roma kutokea Italia.

Na

-Innocent Chambi-

About Innocent Chambi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *