michezo

Loris Karius Aendelea Kupokea Vitisho.

on

Polisi wa eneo la Merseyside, Uingereza wamesema wanafahamu kuhusu vitisho vya maisha ambavyo vimetolewa dhidi ya mlinda lango wa Liverpool Loris Karius baada ya kuchezwa kwa fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumamosi.

Maafisa wamesema vitisho vyovyote vinavyotolewa kupitia mitandao ya kijamii vinafaa kuchunguzwa.

Karius, 24, na familia yake wamekuwa wakipokea vitisho baada ya makosa mawili kutoka kwake kuwasaidia Real Madrid kupata ushindi wa 3-1.

“Tunachukulia ujumbe huu wa vitisho kwenye mitandao ya kijamii kwa uzito sana. Visa hivi vitachunguzwa,” polisi wamesema.

“Maafisa wa polisi wanafahamu kuhusu ujumbe kadha na vitisho vilivyotolewa kupitia mitandao ya kijamii.

“Polisi wa Merseyside wangependa kuwakumbusha wanaotumia mitandao ya kijamii kwamba makosa yooyte yakiwemo kutoa mawasiliano yenye hila na kutumia vitisho, haya yote yatachunguzwa.” Maafisa wa polisi wamesema.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *