siasa

Lowassa, “Nimefurahi Mkapa Ameliibua Hili…Ilikuwa Ni Ajenda Yangu”

on

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Edward Lowassa amemueleza Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa kuhusu kauli yake aliyoitoa hivi karibuni akitaka kuwepo kwa mjadala wa kitaifa kujadili hali ya elimu nchini, kwamba ilikuwa ajenda yake tangu alipokuwa CCM.

Kauli hiyo imetolewa kwa vyombo vya habari na msemaji wake, Aboubakar Liongo jumatatu, ambapo Katika taarifa hiyo, Lowassa amesema suala la elimu pia lipo katika ilani ya uchaguzi ya Chadema.

Katika hafla ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Profesa Idris Kikula, Mkapa alisema kuna janga katika elimu nchini na kushauri kuitishwa kwa mdahalo wa wazi utakaoshirikisha makundi yote ya jamii kwa ajili ya kujadili suala hilo.

Katika taarifa yake hiyo, Lowassa amesema amesoma na kusikia taarifa hiyo ya Mkapa akitaka kuwepo kwa mdahalo wa kitaifa kuhusu kushuka kwa elimu nchini.

“Nimefurahi kuwa Mkapa ameliibua suala hili kwani hiyo ilikuwa ni ajenda yangu ya kwanza tangu nikiwa ndani ya CCM na nje ya CCM. Pia Ilani ya uchaguzi ya Chadema, elimu ndio ilikuwa ajenda kuu na tulisema tutaita mjadala wa kitaifa kuhusu elimu na kuangalia wapi tumekwama na nini kifanyike,” amesema Lowassa.

Lowassa amedai ajenda hiyo sio ya CCM na hawataweza kuisimamia kwa sababu wanataka kuendelea kutawala,ila hawataki Taifa lililoelimika vizuri na linaloweza kuhoji.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *