habari

Lulu Abadilishiwa Kifungo. Sasa Kutumikia Kifungo Cha Nje.

on

Mahakama Kuu ya Tanzania imembadilishia adhabu ya kifungo, Staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, ambaye kuanzia sasa atatumikia kifungo cha nje.

Lulu  Novemba 13 mwaka jana alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake ambaye alikuwa pia mpenzi wake, Steven Charles Kanumba, tukio lililotokea April 7, 2012, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

Lucas Mboje, Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, amesema Lulu amebadilishiwa adhabu hiyo kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam ambapo atatumikia kifungo cha nje.

Amesema pia kwamba, msanii huyo aliachiwa tangu juzi Jumamosi Mei 12, huku akisisitiza kuwa si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, ambayo kisheria inaitwa ‘community service.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *