habari

MAAFISA HABARI WA MAHAKAMA YA TANZANIA WATEMBELEA SHIRIKA LA MAGAZETI YA SERIKALI KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA KUHABARISHA UMMA

on

IMG_9555

Maafisa Habari wa Mahakama ya Tanzania wakiwa katika chumba cha Habatri cha gazeti la HabariLeo walipotembelea Ofisi za Shirika la Magazeti ya Serikali kwa kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika kuuhabarisha Umma. Wa pili kushoto ni Kaimu Mhariri wa gazeti la Habari Leo Bwana Nicodemus Ikonko na wa pili kulia ni Mtaalamu Mwelekezi wa Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Dkt. Cosmas Mwaisobwa, Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Mahakama ya Tanzania Bwn. Nurdin Ndimbe. Wa kwanza kulia ni Afisa Habari Mwandamizi, Lydia Churi na wa kwanza kushoto ni Afisa Habari, Mary Gwera.

IMG_9556

Baadhi ya Waandishi wa Habari wa gazeti la Habari leo na SpotiLeo wakiwa katika chumba chao cha Habari.

IMG_9573

Mhariri wa Makala wa gazeti la HabariLeo Bw. Nelson Goima (kushoto) akiwaelezea Maafisa Habari wa Mahakama ya Tanzania kuhusu utendaji kazi wa gazeti la Habari Leo kwa upande wa uandishi wa Makala.

IMG_9583

Maafisa Habari wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mtaalamu Mwelekezi wakifuatilia jambo wakati wa ziara yao katika Shirika la Magazeti ya Serikali (Tanzania Standard Newspapers) leo

jijini Dar es salaam.

IMG_9587

Mtaalamu Mwelekezi wa Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Dkt. Cosmas Mwaisobwa akimwelezea jambo Mwandishi wa Habari Mwandamizi Rodgers Luhwago katika chumba cha Habari cha gazeti la Daily News.

IMG_9593

Maafisa Habari wa Mahakama ya Tanzania pamoja na wenyeji wao wakizungumza na waandishi wa Habari wa gazeti la Daily News (hawapo pichani)  walipokuwa katika chumba cha Habari cha gazeti hilo.

IMG_9672

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Nurdin Ndimbe akimkabidhi nakala za vitabu vinavyoelezea Mpango Mkakati wa miaka Mitano wa Mahakama, Kaimu Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Bibi. Tuma Abdallah wakati wa ziara ya Maafisa Habari wa Mahakama katika shirika hilo.

IMG_9678

Kaimu Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Bibi. Tuma Abdalah akimkabidhi Fulana Maalum za Shirika hilo Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Nurdin Ndimbe. Pamoja na kutoa zawadi hiyo, Naibu Mhariri Mtendaji pia aliahidi kushirikiana kwa karibu na Mahakama ya Tanzania katika masuala yote yanayohusu kuuhabarisha Umma.

IMG_9685 IMG_9647

Mhandisi Mwandamizi wa Kiwanda cha Uchapaji cha Shirika la Magazeti ya Serikali, David Celestine akiwaelezea jambo Maafisa Habari wa Mahakama walipotembelea katika eneo lake.

IMG_9660 IMG_9601

Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Nurdin Ndimbe akiwaelezea Waandishi wa Habari wa gazeti la Daily News (hawapo pichani) kuhusu Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mradi wa maboresho ya huduma za mahakama jambo katika chumba cha Habari cha gazeti la Daily News.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *