habari

Madaktari Wa Hospitali Ya Temeke Wathibitisha Kumpokea Kijana Aliyejeruhiwa Kwa Risasi.

on

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Temeke Dk Amani Malima, amethibitisha kumpokea kijana Alex Suke (18) anayedaiwa kupigwa risasi na polisi waliokuwa wakituliza vurugu eneo la Buguruni Relini Ijumaa iliyopita.

Dk Malima alisema madaktari wanaendelea kumpatia matibabu na kubainisha kuwa juzi alishindwa kuthibitisha tukio hilo kwa maelezo kuwa hakuwepo ofisini, alisema “Yupo wodi namba saba lakini kamuone Dk Mwita ambaye yuko zamu atakupa ushirikiano,”
Mama wa kijana huyo, Aghata Mwangamba alisema madaktari walimueleza kuwa mwanae atafanyiwa upasuaji wa mkono ambao ulijeruhiwa kwa risasi huku akilalamikia mzigo wa gharama za matibabu. Alisema kuwa, “Leo (jana) analalamika sana mkono tofauti na jana (juzi) na madaktari wameniambia leo (jana) watamfanyia upasuaji mwingine wa mkono ambao ulijeruhiwa na risasi,”
Alisema wameiomba Serikali iwasaidie katika matibabu kwani hadi sasa ametumia Sh900,000 katika matibabu.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwamo Juma Liwanje walieleza kuwa kijana huyo alipigwa risasi kutokana na vurugu zilizotokea eneo la Buguruni Relini baada ya askari kufyatua risasi kuwatawanya watu wakiwamo madereva bodaboda.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *