habari

Madereva 11 Wauawa Kwa Kushambuliwa Na Watu Wenye Silaha.

on

Maafisa wa jeshi la polisi Afrika Kusini wamesema Madereva wa mabasi madogo ya abiria nchini humo  wameuawa baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha.

Watu hao kutoka jimbo la Gauteng walikuwa wakisafiri kwenda Johannesburg usiku wa Jumamosi na kushuhudiwa basi lao likishambuliwa.

Waathirika, na wengine walikuwa wamejeruhiwa vibaya, walikuwa wametoka kwenye mazishi ya mfanyakazi mwenzao katika mji wa pwani wa Kwa-Zulu Natal, Polisi walieleza.

Aidha, Chanzo cha shambulio hilo hakijajulikana ingawa kumekuwa na hali ya uhasama miongoni mwa makundi yanayoendesha Mabasi hayo nchini humo.

Mabasi madogo ya abiria ni maarufu sana miongoni mwa raia wa nchi hiyo wanaofikia milioni 55.

Msemaji wa Polisi Brigedia Jay Naicker amesema basi hilo lilishambuliwa katikati ya mji wa Coleso na Weenen.

”Gari lilishambuliwa, kulikuwa na vifo vya watu 11 na wengine wanne walikuwa wamejeruhiwa vibaya na wamekimbizwa hospitali”, aliwaambia wana habari.

Tukio hili limekuja siku kadhaa baada ya mashambulizi kufanyika Johannesburg,Vyombo vya habari vya Afrika Kusini vimeripoti.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *