habari

Mafuriko Jijini Nairobi Yendelea Kuleta Adha.

on

Mvua kubwa iliyonyesha leo Alhamisi asubuhi imesababisha mafuriko makubwa jijini Nairobi nchini Kenya, na kutatiza watu kufika kazini na magari kukwama. Mvua hiyo iliyoanza saa 12 na nusu asubuhi pia imesababisha msongamano mkubwa wa magari huku watu wakilazimika kupita juu ya maji. Maji yameshuhudiwa yakielekea katika barabara nyingi za katikati ya jiji hilo kubwa la Afrika Mashariki, mafuriko ambayo wakaazi wanasema hawajawahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.

Barabara zilizoathiriwa na mafuriko hayo ni pamoja na Moi Avenue, Tom  Mboya, Racecourse, Ronald Ngala , Haile Selassie Avenue, Temple Road, na barabara ya Kimathi. Barabara kuu ya kwenda mji wa pili kwa ukubwa Mombasa pia imeathiriwa na mvua hiyo na kujaa maji. Mvua kubwa imekuwa ikinyesha nchini Kenya katika siku za hivi karibuni huku mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo ikionya kuwa mvua kubwa itaendelea kushuhudiwa katika siku zijazo.

Wito umetolewa kwa watu katika maeneo ambayo kuna mafuriko, kwenda katika maeneo yaliyoinuka, kuepuka kutembea ndani ya maji na kutoendesha gari katika maji yanayoonekana kutulia.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *