habari

Mafuriko Yamesababisha Madhara Makubwa Kenya.

on

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limesema jumla ya watu 100 wamefariki Dunia kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo.

Shirika hilo limesema Idadi ya watu walioachwa bila makazi imekaribia laki mbili na nusu ambayo ni robo milioni huku shirika hilo likitoa tahadhari kwamba huenda kukazuka magonjwa yanayoenezwa na maji machafu.

Athari hizo za mvua zinaripotiwa kuanza katika miezi ya hivi karibuni, ambapo katika kipindi cha Mwezi march mwaka huu, Baadhi ya maeneo nchini Kenya yaliripotiwa kuathirika vibaya baada ya mafuriko kukata mawasliano ya barabara.

Hata hivyo shirika la Msalaba Mwekundu kupitia ukurasa wake wa Twitter lilisema baadhi ya barabara nchini humo ziliribiwa ikiwemo barabara ya Kajiado-Namanga kusini mwa Kenya, na kufanya eneo hilo kushindwa kupitika.

Kenya ni miongoni mwa Nchi zilizo athirika na mafuriko katika ukanda wa afrika mashariki  ambapo nchi nyingine ni Rwanda na Tanzania. Kwa upande wa Rwanda, taktibani Watu 41 waliripotriwa kufariki dunia kutokana na mafuriko yaliosababishwa na mvua zilizonyesha kwa kipindi cha takriban miezi miwili, huku  Wizara inayohusika na kupambana na majanga ikisema inaendelea kuwaasa raia wanaoendelea kuishi kwenye maeneo hatarishi kuhama.

About Hosea Revocatus

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *