habari

MAGEREZA KUU ARUSHA YAPATIWA NISHATI YA UMEME WA JUA

on

IMG_1200
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizindua Mtambo wa sola uliofungwa na kampuni ya Mobisol Gereza kuu ya Arusha.
Na Vero Ignatus, Arusha.
Gereza kuu la Arusha limepatiwa msaada wa nishati ya umeme jua iliyotolewa na kampuni ya sola ya Mobisol ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika katika Gereza hilo na kuondokana na changamoto ya kukatika kwa umeme Mara kwa Mara.
Mtambo huo wa umeme wa jua umezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambapo amesema kuwa itasaidia kuimarisha usalama kwa wafungwa na askari magereza kwani eneo hilo linahitaji nishati ya uhakika.
Gambo alisema kuwa kampuni hiyo imefanya ubunifu mkubwa wa kuikumbuka magereza taasisi ambayo ilikua ikisahaulika na wadau wa maendeleo.Mmoja wa Waasisi wa Kampuni ya Mobisol Livinus Manyanga alisema kuwa msaada huo ni kutambua changamoto ya nishati iliyopo ila kwa sasa mitambo waliyoiweka itasaidia kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa shughuli za magereza.
“Mitambo hii imegharimu kiasi cha shilingi milioni 16 na tutaihudumia kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu ili kusaidia Wafungwa na Mahabusu wapate mwanga wa uhakika” Alisema Manyanga
Mkuu wa Gereza la Arusha Anderson Kamtyaro wameishukuru kampuni ya Mobisol kwa msaada huo ambao itasaidia kuwezesha magereza na wafungwa kufanya kazi katika mazingira bora ya kazi.Anderson aliwataka Wadau wengine kuiga mfano wa kampuni ya Mobisol kwa kujitoa kutatua changamoto zilizoko kwenye taasisi za serikali.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *