michezo

Majambazi Wamshambulia Manuel Pellegrini.

on

Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini ameporwa na majambazi waliokuwa na bunduki nchini Chile. Mkufunzi huyo maarufu sana duniani ambaye aliwahi kuwa meneja wa mabingwa wa England Manchester City alikuwa njiani kuelekea kwenye mgahawa mmoja mjini mkuu wa Chile, Santiago, akiwa na mke na marafiki wawili pale walipovamiwa.

Msemaji wa West Ham United amesema: “Tuna furaha kusikia kwamba Manuel na mkewe wako salama, hawakudhuriwa.”

Kupitia ujumbe wa Twitter aliouandika kwa Kihispania, Pellegrini amewashukuru polisi wa Chile kwa ujasiri wao na kwa kufika eneo la tukio upesi sana.

Pellegrini, ambaye ni mzaliwa wa Chile, aliteuliwa meneja wa West Ham mwezi Mei.

About Muhammed Khamis

hosearevocatus9@gmail.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *