We have 90 guests and no members online

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akikata utepe kwenye boksi lililokuwa na Mtaala utakaotumia katika mafunzo hayo wakati wa ufunguzi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade (kulia) akionesha mtaala utakaotumika katika mafunzo ya washiriki 150 waliodahiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kushoto ni Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi (ITA) Prof. Isaya Jairo

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade(wa sita kutoka Kulia) na Mkuu wa Chuo cha uongozi wa Kodi Prof. Isaya Jairo (ITA) (wa Tano kutoka kushoto) wakiwa katika Picha ya Pamoja na washiriki wa Mafunzo hayo baada ya kuyazindua leo Jijini Dar es Salaam.

Posted On Monday, 13 April 2015 13:48

Meneja Mdhibiti Viwango wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Conchesta Ngaiza (kulia) akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Raymond Wisenge. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.

Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Calvin Martin akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.

Mshauri wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Phocus Lasway akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe (kulia) wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Raymond Wisenge. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake. (Muro)

Posted On Monday, 13 April 2015 13:39

images

Na Bashir Yakub.

Ukisoma kichwa cha habari utaona nimeongelea nyumba lakini kimsingi mchakato huu unahusisha mali zote za wanandoa vikiwemo viwanja, magari, na kila kitu ambacho ni mali ya wanandoa. Kichwa kinajieleza kuwa ni makosa benki au taasisi yoyote ya fedha kuuza nyumba au mali yoyote ya wanandoa ikiwa wakati wa kuchukua mkopo mwanandoa mmojawapo hakushirikishwa katika mchakato wa mkopo huo.

1. MAANA YA MALI YA WANANDOA.
Mali ya wanandoa ni mali yoyote ambayo imepatikana kwa nguvu au juhudi za pamoja kati ya mme na mke walio kwenye ndoa ya kikristo, kiislam, ya serikali au ndoa nyingine yoyote halali ikiwemo ile ya kuishi wote kwa muda wa miaka miwili ( presumed marriage ).

Hizi zote ni ndoa ambazo mali ikipatikana ndani yake huwa ya wanandoa. Pia ile mali ambayo mmoja wa wanandoa amekuwa nayo kabla ya ndoa lakini baada ya ndoa ikaendelezwa na wanandoa kwa kiasi kidogo au kikubwa nayo hubadilika kuwa ya wanandoa wote.

Hii inajumuisha mali zilizopatikana kabla ya ndoa lakini wanandoa wenyewe wakaamua kwa hiari yao kuzifanya kuwa zao wote kwa pamoja kama familia kwa makubaliano maalum. Nalazimika kutoa ufafanuzi huu ili ninaposema mali ya wanandoa hairuhusiwi kuuzwa ieleweka hata kwa kiwango kidogo mali zipi ni za wanandoa na hivyo kuhitaji ridhaa ya wote katika kuwekwa dhamana.

Posted On Monday, 13 April 2015 06:16

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akipanda mti kuashiria maadhimisho ya upandaji miti kimkoa yaliyofanyika katika eneo la Gereza la Kigongoni wilayani Bagamoyo.

Na John Gagarini, Bagamoyo

MKOA wa Pwani umefanikiwa kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni nane kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika kipindi cha mwaka 2013/2014.

Hayo yalisemwa juzi wilayani Bagamoyo na Ofisa Misitu wa mkoa huo Daniel Isara, wakati wa maadhimisho ya upandaji miti kimkoa iliyofanyika kwenye eneo la la Gareza la Kigongoni ambapo ilipandwa zaidi ya miti 3,000.

Isara alisema kuwa fedha hizo zimetokana na kukabiliana na uharibifu wa rasilimali misitu na mazingira ambapo doria ziliimarishwa na ukusanyaji wa mapato kufikia kiasi hicho.

Alisema kuwa hadi kufikia mwezi Januari 2014/2015 makusanyo yalifikia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni sita baada ya wakala hao kuongeza watumishi kwenye ngazi za wilaya.

Posted On Saturday, 11 April 2015 10:25

Mkurugenzi huduma na elimu kwa mlipa kodi,Richard Kayombo akizungumza leo na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akiwataka wananchi kutoa taarifa ya bidhaa zinazosafirishwa kwa njia za magendo, katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO,jijini Dar es Salaam. kushoto ni Meneja elimu kwa mlipa kodi,Diana Masala na kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idaya ya habari Maelezo Zamaradi Kawawa.

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA), kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita imekusanya zaidi ya Sh. Bilioni 258 zilizotokana na faini ya bidhaa mbalimbali za magendo.

Hayo ameyasema leo Mkurugenzi huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam,amesema TRA inaungana na jeshi la

Polisi katika kukamata watu wanaojihusisha na usafirishaji na uuzaji wa bidhaa za magendo ambazo zinaisababishia serikali kukosa mapato.

Amesema kwa Mkoa wa Kagera zaidi ya Sh.milioni 120 zilizotokana na pombe ya aina ya signature Vodka katoni 2043 kutoka nchini Uganda sawa na lita 24,516 yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 61, zilizosafrishwa kwa jahazi la MV Tabasamu lenye namba za usajili MTZ 0541.

Hata hivyo amesema Mkoa wa Morogoro kodi ya zaidi ya Sh.milioni 66 ilipatikana baada ya kukamata madumu 1599 ya lita 20 za mafuta ya kupikia yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 65ambapo wakwepa kodi hao walilipa faini pamoja na kodi waliyokuwa wakikwepa na Mkoa wa

Tanga madumu 888 ya mafuta ya lita 20 yalikuwa na thamani ya zaidi ya sh.milioni 15 yaliyokamatwa eneo la Kwame katika bandari bubu ya wilayani Mkinga.

Kayombo amesema katika Mkoa wa Arusha jumla ya lita 2290 za mafuta ya taa zenye thamani ya zaidi ya sh.milioni mbili,mafuta hayo yalikuwa yakisafirishwa kwa gari aina ya Toyota hiace iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Holili Kwenda Mkoani Moshi. (Muro)

Posted On Friday, 10 April 2015 16:21

Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mohamed Lukwele kushoto akiwa na Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko wa kampuni ya Selcom, Juma Mgori na Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta wakati wa uzinduzi wa mashine ya ukusanyaji wa kodi kwa njia za kielektronic mkoa wa Morogoro

Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta kushoto akimwelekezaKaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Bakari Sagini jinsi ya kutumia mashine ya ukusanyaji wa kodi kwa njia za kielektronic wakati wa uzinduzi rasmi wautumiaji wa mashine hizo kwa Manspaa ya Morogoro

Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta kushoto akimwelekeza Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mohamed Lukwele jinsi ya kutumia mashine ya ukusanyaji wa kodi kwa njia za kielektronic wakati wa uzinduzi rasmi wautumiaji wa mashine hizo kwa Manspaa ya Morogoro Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko wa kampuni ya Selcom, Juma Mgori katikati akitoa mahelezo ya mashine ya ukusanyaji wa kodi kwa njia za kielektronic wakati wa uzinduzi rasmi wautumiaji wa mashine hizo kwa mkoa wa Morogoro kulia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mohamed Lukwele na Meneja miradi wa Selcom Gallus Runyeta. (Muro)

Posted On Friday, 10 April 2015 05:20

Mwenyekiti wa ALAT taifa na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam - Dr Didas Masaburi akitangaza maadhimisho ya mkutano mkuu wa 31 wa ALAT -2015. Pembeni ni Afisa Mkuu Fedha wa NMB – Waziri Barnabas na Katibu Mtendaji wa ALAT - Bw. Abraham Shamumoyo.

Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas akikabidhi mfano wa hundi kwaajili ya udhamini wa mkutano mkuu wa ALAT – 2015 kwa mwenyekiti wa ALAT taifa na meya wa Jiji la Dar es Salaam Dr Didas Masaburi . Katikati ni Katibu Mtendaji wa ALAT – Bw Abraham Shamumoyo.

Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas akitangaza udhamini wa NMB katika mkutano mkuu wa ALAT Taifa mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Karijee jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa ALAT taifa na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam - Dr Didas Masaburi na pembeni ni Katibu Mtendaji wa ALAT - Bw Abraham Shamumoyo.

Posted On Friday, 03 April 2015 07:22

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),kutokaTanzania Dkt. Albina Chuwa akifungua mkutano wa Wakurugenzi na Watalaam wa Takwimu kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili mausuala mbalimbali ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Uganda Bw. Ben Mungyereza akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwi mu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashari kikuhusu utayari wa nchi yake katika matumizi ya Takwimu mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Rwanda Bw. Yusuf Murangwa akitoa mchango wake kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa matumizi ya Takwimu baina ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.

Posted On Friday, 03 April 2015 06:56

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga (Kushoto) na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini unaoanza tarehe 01 hadi tarehe 02, Aprili 2015 wenye lengo la kujadili mafanikio na changamoto katika utendaji kazi wa Wizara pamoja na taasisi zake.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE) Wizara ya Nishati na Madini, Marcelina Mshumbusi akisoma hotuba ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (hayupo pichani) katika mkutano huo. Kushoto ni Katibu wa TUGHE Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini.

Posted On Wednesday, 01 April 2015 17:53

ndugai31_fa5e9.jpg

Naibu spika Job Ndugai

WABUNGE wameitaka Serikali kuharakisha mazungumzo yake kuhusu tatizo lililopo la mgomo wa wafanyabiashara nchi nzima, ili suala hilo lipatiwe ufumbuzi mapema.

Hayo yalibainishwa bungeni hapo na Naibu Spika Job Ndugai, wakati wakati akijibu miongozo mbalimbali iliyoombwa na wabunge kuhusu suala hilo ambao wengi wao walitaka mijadala ya Bunge hilo iahirishwe ili suala hilo lijadiliwe kama dharura.

Hata hivyo, Ndugai alisema kutokana na hali halisi iliyopo sasa ni muhimu mazungumzo hayo yakaendeshwa kwa haraka ili kufikia mwafaka na kupata ufumbuzi wa mgogoro uliopo.

Posted On Wednesday, 01 April 2015 03:28

Mh.Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Harrison Mwakyembe akihutubia wajumbe wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango unaofanyika Mjini Addis Ababa –Ethiopia.

Naibu Katibu Mkuu –Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Nd. Armantius C.Msole (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr.Hamisi Mwinyimvua wakifuatilia hotuba ya Mh.Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr.Harrison Mwakyembe (Hayupo pichani) katika Ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango wa Afrika unaofanyika Mjini Addis ababa – Ethiopia.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dr.Hamisi Mwinyimvua akipata maelezo kuhusu utaratibu wa Mkutano kutoka kwa kamishina msaidizi wa Fedha za nje Bi.Judica Omari baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Fedha,Uchumi na Mipango unaoendelea Mjini Addis Ababa – Ethiopia. Katikati ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr.Albina Chuwa.(Muro)

Posted On Tuesday, 31 March 2015 07:40

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad akizungumza wakati wa kukabidhi Ripoti yake Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Akimkabidhidhi Ripoti yake Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad(kushoto)ikulu jijjini Dar es Salaam leo.Kulia anayeshuhudia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika

Posted On Friday, 27 March 2015 16:43
Page 8 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi