We have 85 guests and no members online

×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 641

Moja ya changamoto kubwa inayoikabili jamii yetu,ni kutotimiza majukumu kama yalivyokubaliwa. Yawe tuliyopewa au tuliyojiwekea sisi wenyewe. Kwa upande wa biashara, iwe ni kubwa ama ndogo, ni dhahiri kuwa kutakuwa na majukumu mengi yanayotakiwa kufanyika kila siku kwa ubora uliokubaliwa.

Swali unalotakiwa kujiuliza, je unatumia mtindo upi kuchunga majukumu na kufuatilia muenendo wake? Pia haujawahi kujiuliza, ni tatizo gani linaweza kusababisha kuchelewa ama kutokukamilika kwa jukumu fulani? Na je, hakuna njia yoyote itakayoweza saidia kwenye kuchunga muenendo wa majukumu?

Posted On Wednesday, 04 March 2015 10:25

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.
BENKI ya CRDB imezindua kampeni maalum ya utumiaji wa huduma zake kupitia simu za mkononi 'SimBanking' kupitia kwa mawakala wa 'FahariHuduma'.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama 'Tuma Pesa na SimBanking Shinda Passo', Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei alisema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kuwakumbusha wateja wake na watanzania wote kwa ujumla umuhimu wa kutumia njia hizo mbadala ili kupata huduma kwa urahisi na uharaka.

Alisema kampeni hiyo inatarajiwa kutoa magari kumi na mbili ambapo kila mwezi mshindi mmoja atazawadiwa gari hilo, pamoja na zawadi ya gari la wateja watakaotumia huduma hizo pia wataweza kujishindia zawadi nyingine mbalimbali zikiwemo solar power, tables na simu za kisasa za mkononi.

"Tunataka kuwavutia wateja wetu kuziamini na kuzitumia zaidi huduma hizi kwani ni sawa kabisa na kupata huduma kupitia matawi yetu,".

Akielezea namna ya kushiriki na jinsi mshindi atakavyopatikana, Dk. Kimei alisema kuwa shindano hilo ni la wateja wote wa CRDB watumiao huduma hizo na mshindi atakuwa ni yule mwenye miamala mingi zaidi kwa mwezi husika.

Posted On Friday, 30 January 2015 04:33

 

Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Mkuu wa Kongane ya Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kiuchumi, Bw. Paul Sangawe (Kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory).

Mtaalamu wa Masuala ya Forodha kutoka TRA, Bw. Stambuli Myovela (Kulia) akizungumza wakati wa Semina ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory) kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

Posted On Monday, 26 January 2015 11:26

bei-petroli_7ba43.jpg

BEI ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, imeshuka kuanzia leo, huku watumiaji wa petroli wakipata nafuu zaidi kutokana na kuuzwa chini ya Sh 2,000 baada ya kipindi cha muda mrefu.

Kutokana na kushuka kwa bei ambako pia kunachangiwa na kushuka kwa bei katika soko la dunia, sasa petroli itauzwa lita moja kwa Sh 1,955, dizeli itakuwa Sh 1,846 kwa kila lita moja na mafuta ya taa yatakuwa yanauzwa kwa Sh 1,833 kwa kila lita moja.(MM)

Posted On Wednesday, 07 January 2015 08:48

DSC03176

Miss Singida 2014 Dorice Mollel akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwenye wodi ya watoto njiti ya hospitali ya mkoa mjini Singida. Miss Singida huyo ambaye mwaka jana alikuwa pia mshindi wa kwanza Miss kanda ya kati na kushika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema ametoa msaada huo kwa sababu na yeye alizaliwa mapacha njiti.

Na Nathaniel Limu, Singida

JUMLA ya watoto 284 hadi 300, huzaliwa kila mwaka katika hospitali ya mkoa iliyopo mjini Singida wakiwa hawajatimiza umri wa kawaida wa kuzaliwa (njiti).

Kati ya watoto hao,inakadiriwa 60 hadi 83 hufariki kutokana na sababu mbalimbali kila mwaka ikiwemo ya tatizo la kupumua.

Posted On Sunday, 04 January 2015 04:43

NesiWangu Show ni kipindi kinachokusudia kuongeza mwako katika uwanja wa Afya, upatikanaji wa huduma zake na elimu-afya kwa jamii.

Katika kipindi hiki, tunazungumza na Mkurugenzi wa Jenga Tanzania Foundation, Nassor Basalama anayezungumzia kuhusu kipimo cha Malaria ambacho Jenga Tanzania Foundation inapanga kukisambaza bure kwa watu wa kipato cha chini nchini Tanzania.
Karibu uungane nasi

                                                                                              VICTOR SIMON

Posted On Monday, 29 December 2014 06:05

Kila tarehe 19 mwezi Novemba huwa ni maadhimisho ya siku ya choo duniani, kwa hiyo mjengwablog inasisitiza na kukumbusha umuhimu wa matumizi sahihi ya choo katika jamii ili kutunza usafi wa mazingira na kuepuka magonjwa yatokanayo na ukosefu wa vyoo bora.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu,ni Choo bora na mikono safi kwa afya bora,heshima na usawa".(Martha  Magessa)

Posted On Wednesday, 19 November 2014 09:05

Displaying 01.JPG

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.

Displaying 02.JPG

Mwandishi wa habari wa Redio Adhana Harith Subeit akitaka ufafanuzi kutoka kwa viongozi wa Wizara ya Afya kuhusu maadhimisho ya siku ya kisukari Duniani kwenye mkutano uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.

Displaying 03.JPG

 Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Mohd Dahoma akijibu maswali ya waandishi wa Habari kuhusu maadhimisho ya siku ya kisukari katika mkutano uliofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja.(Martha Magessa)

Posted On Saturday, 15 November 2014 08:32

Displaying afya 255.jpg

Displaying afya 249.jpg

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Stephen Kebweleo kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo akitoa tamko kuhusu Siku ya Kisukari Duniani itakayoadhimishwa Novemba 14, mwaka huu duniani kote.Kushoto ni Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dkt. Ayoub Magimba.Picha na Magreth Kinabo.(Martha Magessa)

Posted On Friday, 14 November 2014 10:38

Displaying 01.jpg

Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumuko wa bei nchini.

Displaying 03.jpg

Baadi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumzia suala la mfumuko wa bei nchini.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)(Martha Magessa)

Posted On Monday, 10 November 2014 07:53

unnamed

Mwakilishi wa naibu mkurugenzi mkuu wa NHIF Bwana Michael Kishiwa (mwenye koti jeusi) akimkabidhi  Mkuu wa wilaya ya Musoma Mh. Jakson Msome  vifaa tiba, kwa ajili ya matumizi ya hospitali hiyo ya mkoa wa mara.

unnamed5

Wananchi na wagonjwa wakifatilia kwa makini zoezi zima la makabidhiano ya vifaa tiba lililokuwa ikiendelea meza kuu

unnamed7

(Martha Magessa)

Posted On Thursday, 06 November 2014 08:15

Na Anita Jonas-MAELEZO

Umoja wa Mataifa umeshauri kuchukua hatua za haraka kwa magongwa ya mlipuko yanayotokea Afrika kama Ebola kwani yanadhiri uchumi wa mataifa husika.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka wakati wa Maadhimisho ya Miaka 69 ya Umoja wa Kimataifa leo Jijini Dar es Salaam.(Martha Magessa)

Posted On Saturday, 25 October 2014 06:32
Page 9 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi