We have 84 guests and no members online

×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 641

pix 1-day 2

Wadau wa madini ya vito kutoka sehemu mbalimbali duniani, wakipatiwa huduma katika Banda la Tanzania katika Maonesho ya 54 ya Kimataifa ya Vito na Usonara – Bangkok, Thailand.

pix 6-day 2

Mfanyabiashara wa madini ya vito kutoka Tanzania, Latifah Abdallah akitoa maelezo kuhusu madini hayo kwa wadau waliotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok.

pix 8-day 2

Baadhi ya Washiriki kutoka Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok wakipozi kwa picha muda mfupi kabla ya kuanza  kwa siku ya tatu ya maonesho hayo. Kutoka Kushoto ni Asimwe Kafrika, Iddi Pazzi, Gregory Kibusi, Nelson Magawa, Teddy Goliama na Matiko Sanawa.

Posted On Friday, 12 September 2014 04:52

Katika maendeleo ya jamii yoyote, moja ya kitu muhimu ni kukuwa kwa maarifa ya wanajamii. Maarifa yatakayowapa uwezo wa kutumia ujuzi kwenye kutenda. Haijalishi upo kwenye fani gani, bali siku ya mwisho ni lazima uweze kutenda na siyo kuishia vitabuni.

 Kwa miaka mingi, nimekuwa nikifuatilia tatizo la ajira, umasikini nk hapa nchini, ingawa kuna mambo mengi sana ndani yake, lakini mzizi wa yote ni maarifa. Kizazi chetu SIYO kizazi cha watu wenye maarifa. Hii inawezekana ni kutokana na uvivu wa kujifunza au kutokuwa na nyenzo za kujifunza. Na kwakuwa na kizazi cha watu wasio na maarifa, kinapelekea kurudisha nyuma mambo mengi sana.

 Leo hii, kazi nyingi zinafanywa nje ya nchi, hata Toothpick tunaagiza kutoka nje, leo hii ukienda Supermarket zaidi ya asilimia tisini ya vitu, vinatoka nje. Sasa, swali la kujiuliza je hapa nyumbani hatuna watu wenye uwezo wa kutenda? Jibu, ni tunao, ila ni wachache na kasumba yetu inatuumiza pia wengi hawajiamini.

Posted On Friday, 05 September 2014 08:49

Katika dunia hii ya utandawazi, ushindani ni kitu kisichoepukika. Haijarishi wewe unafanya biashara ya kuuza peni au una blogu yako au hata unauza dhahabu. Utandawazi umeweza kuwafanya wanunuzi wawe na sauti na machaguo mengi toka kila pande, pande hizi zinaweza kuwa hata nje ya mipaka ya nchi. Pia, wanunuzi wamepewa uwanja mkubwa wa kuijadili na kupata taarifa za biashara yako kwa urahisi zaidi, mitandao jamii ni moja ya kitendea kazi kwenye hili.

Ingawa ushindani ni mkubwa sanasana, lakini leo hii, kama utatembelea kwenye biashara kadhaa nchini Tanzania, utakubaliana na mimi kuwa, wengi tunafanya biashara kwa mazoea (business as usual)na ubunifu umekuwa mdogo sana kwa makampuni mengi sana. Iwe ya serikali au hata ya watu binafsi, iwe madogo yaliyoanza jana au hata yale yenye umri wa miongo.

Posted On Monday, 01 September 2014 12:00

website Design & Hosting in Tanzania

Siku hizi ni kitu cha kawaida kuona vitu vya ajabu vikitumwa tokea akaunti ya mtu unayemuamini sana na haukutegemea kama mtu kama yeye angeweza kutuma (post) vitu kama hivyo, na ikakufanya hata utake kujitoa (Unlike / Unfriend) toka kwenye urafiki au ufuatiliaji kwake. Je unadhani ni kweli kila kitu kinachotumwa kwenye Facebook hutumwa na na muhusika? Jibu ni hapana. Mara nyingi ni wavamizi walioingia kwenye akaunti ya muhusika na kuitumia kadri wawezavyo ama kwakuwa umeruhusu vipachiko (apps) zitume kwa niaba yako.

Siku hizi, uvamizi wa akaunti kwenye Facebook umekuwa mkubwa, na asilimia kubwa ya uvamizi huu hutokana na ama wahusika kutofahamu athari wa wanachokichagua ama kutokujua jinsi ya kujilinda. Kama ilivyo ada, Dudumizi itakuelezea namna ya kujilinda na uvamizi huo kwenye Facebook.

Posted On Tuesday, 26 August 2014 08:10

Mgonjwa wa Ebola akipata matibabu nchini Guinea

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuweko na ugonjwa wa Ebola kwenye jimbo la Equateur. Waziri wa afya amesema kwamba watu 2 miongoni mwa 13 waliofariki wiki iliyopita wamekutwa na virusi vya Ebola

Watu wawili wamefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola kwenye eneo la Djera mtaani Boende, jimboni Eqauateur. Waziri wa kongo wa afya, Felix Kabange alyietoa taarifa hiyo amesema kwamba uchunguzi ulioendeshwa na wataalamu wa magonjwa ya kuambukiza kwenye taasisi ya utafiti, unaelezea kwamba watu hao, mmoja alikuwa na virusi vya aina ya Sudan na mwengine mchanganyiko wa virusi vya Sudan na Zaire aina mbili ya virusi vya ugonjwa wa Ebola.

Posted On Tuesday, 26 August 2014 01:52

140824005322 ebola detector 512x288 afp2 a60db

Serikali ya Japan imesema iko tayari kutoa dawa waliotengeneza ya kupambana na homa kali iitwayo T-705 ambayo huenda ikasaidia katika vita vya kupambana na Homa ya EBOLA.
Matumizi ya dawa hiyo hayajaidhinishwa na shirika la afya duniani World Health Organisation, haijabainika iwapo itafaa kutoa afueni kwa wagonjwa wa Ebola au la .(Hudugu)

Posted On Monday, 25 August 2014 14:09

Displaying 589hotel.pic 5 (2).jpg

Moses Mashalla

Mahakama kuu nchini kitengo cha biashara kanda ya Arusha imemuamuru mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa hoteli ya Snowcrest ya jijini Arusha,Wilfred Tarimo pamoja na familia yake kumlipa jumla ya $ 1.7 sawa na zaidi ya sh,3 bilioni mkurugenzi wa kampuni ya Grand Alliance Ltd,James Ndika kama malipo ya awamu ya kwanza ya kununua hisa ndani ya hoteli hiyo.(Martha Magessa)

Posted On Monday, 25 August 2014 05:50

Picha TANSORT

Imeelezwa kuwa Tanzania inatarajia kuwa kitovu kikuu cha madini ya vito barani Afrika baada ya kubainika kuwa na utajiri mkubwa wa madini ya vito.
Hayo yalisemwa na mtaalamu wa madini ya vito na almasi kutoka Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Vito na Almasi (TANSORT) kilicho chini ya Wizara ya Nishati na Madini Teddy Goliama kwenye semina iliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda, Afisa Madini Wakazi na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini inayoendelea mjini Bagamoyo
Goliama alisema Tanzania kupendekezwa kuwa kitovu kikuu cha madini ya tanzanite ni matunda ya ziara iliyofanywa na Kitengo cha TANSORT kwa kushirikisha wataalamu wa wizara ikiwa ni pamoja na ushiriki wake katika maonesho ya kimataifa ya vito ya Thailand yajulikanayo kama Bangkok Gem and Jewellery Fair
Alisema sababu zilizopelekea Tanzania kupendekezwa kuwa kitovu cha biashara ya madini ya vito Afrika ni kutokana na wingi na aina mbalimbali za madini hayo pamoja na madini hayo kupendwa na wafanyabiashara wengi kutoka Thailand na nchi nyinginezo duniani.
Alisema awali Waziri Mkuu wa Thailand aliitembelea nchi ya Tanzania na kukutana na Serikali pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini na kukubaliana maeneo ya kushirikiana ambapo aliahidi kuisaidia Tanzania katika kukuza biashara ya madini ya vito.
Goliama aliendelea kusema kuwa Waziri Mkuu huyo aliikaribisha Tanzania kutembelea Thailand pamoja na kukutana na wataalamu wa sekta wa madini wa nchi hiyo ambapo ujumbe wa wataalamu wa madini ukiongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia madini Mh. Stephen Maselle ulitembelea nchi ya Thailand na kukutana na uongozi wa chama cha wafanyabishara wa madini Thailand unaoshirikiana na Serikali ya Thailand bega kwa bega.
Alisema kuwa moja ya mikakati ya kukuza biashara ya madini ya vito iliyowekwa ilikuwa ni kutoa fursa kwa nchi ya Tanzania kushiriki katika maonesho ya kimataifa ya Bangkok Gem and Jewellery Fair ambayo hufanyika mara mbili kwa mwaka, Februari na Septemba.
Alisisitiza kuwa mara baada ya Tanzania kufanya vizuri katika maonesho hayo na kubainika kuwa na hazina kubwa ya madini ya vito ilipendekezwa kuwa kitovu cha biashara ya madini hayo barani Afrika.
“ Mpaka sasa kwa bara la Afrika hakuna kituo cha biashara ya madini ya vito, maonesho ya Arusha Gem Fair yamekuwa yakitumika kama njia ya kuwakutanisha wafanyabiashara mbalimbali barani Afrika.’’ Alisisitiza Goliama
Aliendelea kusisitiza kuwa Tanzania imeweka mkakati wa kuboresha maonesho yao kuwa ya kimataifa zaidi barani Afrika na kukutanisha wafanyabiashara kutoka mabara mengine duniani pamoja na kuwa kituo kikuu cha madini barani Afrika.
Akizungumzia mchango wa biashara ya madini ya vito nchini Thailand, Goliama alisema kuwa biashara hiyo ni ya tatu katika kuchangia pato la nchi ya Thailand.
Wakati huo huo akizungumzia biashara ya madini ya vito inavyofanyika mtaalamu mwingine kutoka TANSORT Sanawa Matiko alisema kuwa biashara ya madini ya vito mara nyigi inafanyika kwenye maonesho ikihusisha kukutanisha wafanyabiashara yaani wauzaji na wanunuzi wa madini hayo.
“ Maonesho hayo hutumika kama njia moja wapo ya kujenga mtandao wa kibiashara pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji katika madini ya vito nchini’’ alisema Matiko
Matiko aliendeTANZANIAea kusema kuwa mara nyingi maonesho ya kimataifa hutumika kwa wafanyabishara kupata taarifa mpya (updates) za biashara ya madini ya vito pamoja na vifaa vya kisasa kwa ajili ya madini ya vito vilivyogunduliwa na taasisi zinazotengeneza vifaa hivyo.
Akizungumzia biashara ya madini kwa upande wa Tanzania Matiko alisema Tanzania inatakiwa kutumia heshima kubwa iliyopewa kwa kutangaza zaidi madini yake hususan ya vito ndani na nje ya nchi ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi.

 

A.I

Posted On Friday, 15 August 2014 10:46

Tanzania imesema haina mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola.

Kauli hiyo inakuja baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo.

Posted On Friday, 15 August 2014 05:21

 

Picha Na. 1

Rais Mstaafu wa Awamu ya  Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa (kulia) akisisitiza jambo  wakati wa mazungumzo na  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele (Kushoto) aliyemtembelea ofisini kwake

 

Picha Na  2

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa (Kulia) akiwa kwenye mazungumzo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam

Na. Awadh Ibrahim wa Mjengwa Blog/Kwanza jamii radio

Posted On Thursday, 14 August 2014 12:21

 

m4
Rais wa Vijana Wanasayansi Duniani Bw. Meng Wang akitoa maelezo machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kufunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
m5
Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Stephen Masele akiwahutubia Vijana Wanasayansi Duniani wakati alipokuwa akifunga Kongamano la Tatu la Wanasayansi Vijana Duniani lililofanyika Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.


Na Awadh Ibrahim wa Mjengwa Blog/Kwanza jamii radio
Posted On Thursday, 14 August 2014 12:12

DSC_0534

Diwani wa kata ya Ololosokwani na Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Bw. Yannick Ikayo Ndoinyo akiangalia kitanda cha kujifungulia wakimama kwenye Zahanati ya Sero ambayo kwa siku inatibu wagonjwa 50 na zaidi ikiwa na daktari mmoja huku wakazi wanaofuata huduma hiyo kutoka kata hiyo na ya jirani Soitosambu kutembea umbali mrefu kwa Kilometa 7-15 kupata huduma ya afya.(Picha Zainul Mzige wa MOblog)

DSC_0532

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro

Wakazi wa vijiji vya Ololosokwan, Soit-Sambu, Njoroi na Loipir kata za Ololosokwana na Soit-Sambu wilayani Ngorongoro wanakabiliwa na changamoto kubwa ya huduma ya Afya kwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye kijiji cha Sero huku waathirika wakubwa ni kinamama na watoto.

Umbali wa zahanati hizo imekuwa sababu kubwa ya vifo hususani kwa akina mama wajawazito wanaotaka kwenda kujifungua na watoto halikadhalika wanapozidiwa hufia njiani kutokana na umbali wa zahanati kutoka kijiji kimoja kwenda kingine wanapotakiwa kuwahishwa hospitalini hali inayowafanya kutembea umbali mrefu kilometa 15 hadi kuipata huduma ya zahanati .

Akizungumza na waandishi wa habari Diwani wa kata ya Ololosokwani na Mkurugenzi wa Irkiramat Foundation (RAMAT) Yannick Ikayo Ndoinyo waliotembelea miradi inayofadhiliwa na Shirika la Elimu na Sayansi (UNESCO) wilayani humo alisema serikali haina budi kutimiza ahadi yake ya kujenga Zahanati kwa kila kata nchini Tanzania kuwapunguzia wagonjwa hususan akina mama waja wazito na watoto adha ya kutembea au kusafiri mwendo mrefu kutafuta huduma za afya.(Martha Magessa)

Posted On Thursday, 14 August 2014 05:53
Page 10 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Watumishi