We have 172 guests and no members online

Chombo cha NASA na taarifa zasayari za PlutoWana sayansi wa NASA kutoka Marekani wanasema kuwa majaribio yao ya kurusha chombo kwenda katika sayari ya Pluto yamekuwa na mafanikio makubwa.

Chombo hicho kimefanikiwa kutuma taarifa katika kituo cha utafiti huo cha Maryland zilizochukua takribani saa nne na nusu hadi kufika duniani na kupokelewa na antenna NASA.

Saa chache zijazo wanasayansi hawa wa NASA wameeleza kuwa wanatarajia kupata mfululizo wa taariza zaidi na picha kutoka sayari hiyo ya Pluto ambazo zitatoa uhalisia wa undani wa sayari hiyo ya Pluto.CHANZO:BBC

IMECHOTWA KWENYE MTANDAO NA VICTOR SIMON

Posted On Wednesday, 15 July 2015 06:49

1

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akiwaeleza wajumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi kuhusu kuanza kutumika kwa sheria mpya ya Kodi ya ongezeko la thamani ya mwaka 2014 iliyoanza kutumika kuanzia Julai 1, 2015 na jinsi itakavyobadilisha baadhi ya mifumo ya kibiashara,wakati wa Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) Leo Jijini Dar es Salaa.

2

Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi Bw.Nicholus Duhia akimshukuru Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade kwa kuhudhuria ufunguzi wa semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) na kuahidi kuwa washiriki wazuri katika mabadiliko katika sekta ya Kodi nchini,wakati wa Semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) Leo Jijini Dar es Salaa.

3

Baadhi ya wajumbe wa semina ya pamoja Kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) wakimsikiliza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade.(VICTOR)

Posted On Saturday, 11 July 2015 16:17

sage

With smartphone penetration ramping up across Africa, the continent’s businesses have an opportunity to use mobile technology to become more efficient, productive, and responsive in the way they do business.

According to the Ericsson Mobility Report for 2015 (http://www.apo.af/uwS8Ft), there were more than 910 million mobile subscriptions in Africa by the first quarter of 2015. A growing number of these mobile users are now walking around with powerful smart devices that give them access to apps and information wherever they are. 

2264-150701s1

Daryl Blundell – GM, Sage Pastel Accounting.

Download biography Daryl Blundell: http://www.apo-mail.org/Daryl-Blundell.docx

ERP – making collaboration easy

And that, in turn, creates new ways for organisations to interact with employees, suppliers, and other stakeholders. “We’re seeing many organisations mobilise their enterprise resource planning (ERP) software, “says Keith Fenner, Senior Vice-President Sales – Sage ERP Africa & Sage ERP X3 AAMEA, Director and Head of Sage Middle East (http://www.sage.com).

“Workers and managers are increasingly able to access ERP data on the road to serve customers, speed up decision-making, and save time.”

For example, a salesperson can now easily check from a tablet or smartphone whether a product is in stock while on-site with a customer, says Fenner. They can capture the customer’s details and initiate the order without leaving the customer premises, all leading to a faster and more seamless service.

“Mobile workers can now use their time between meetings and at airports more productively,” he adds. “And they can access data on the spot so that they can react to opportunities and problems more rapidly. Of course, mobilising business processes also streamlines processes by allowing data to be captured in the field.”

Posted On Friday, 03 July 2015 06:49

tzNIC-Post

Shirika la tzNIC ni shirika la kitanzania, linalo endeshwa na watanzania ila lisilo la kiserikali. tzNIC inakuwezesha kusajili domain ya tovuti yako ya .tz. Na hivyo basi tzNIC kwakuwa asasi isiyo ya kutafuta faida bei zao ni ndogo sana hivyo kukuwezesha Mtanzania wa kawaida kabisa kuwa na domain ya .tz. Hivyo pale unapo taka kusajili domain ambayo inaishia na .tz hawa ndio wahusika wakuu ambao wametoa vibali kwa wasajili zaidi ya 43 ambao wako Tanzania nzima. Lengo kuu la tzNIC ni kukuza matumizi ya majina ya domain yanayo ishia na .tz pamoja na kulinda maslahi ya walio sajiliwa kwa kuwapa database ambayo ina ulinzi wa kutosha na unafuu. Zaidi sana iwapo kuna tatizo lolote la kisheria unapokuwa na domain ya .tz tatizo hilo linatatuliwa hapa hapa Tanzania na tzNIC. Sajili leo kwa kupitia wasajili walio pewa vibali na tzNIC walioko karibu na wewe kwa kubofya hapa kwa Shilingi 25,000 tuu.

Kwa maelezo zaidi, au hata kama ukitaka ku register domain yako watembele mtandanoni:

Website; http://www.tznic.or.tz/

Facebook; https://www.facebook.com/tznic

Twitter; https://twitter.com/tznic

Posted On Friday, 03 July 2015 06:41

Kundi la watu 21, wakiwemo, wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari yao ya kupanda Mlima Kilimanjaro Juni 22, 2015

Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Acacia, Brad Gordon, (katikati), akiwa na Meneja Mkuu wa Uendelezaji wa kampuni hiyo, Asa Mwaipopo, (kushoto), akizungumza muda mfupi kabla ya kuongoza timu ya wapanda mlima Kilimanjaro kwa nia ya kukjsuanya fedha hizo

Brad, (kushoto), akijadiliana jambo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Necta Pendaeli Foya (katikati)

KAMPUNI ya ACACIA inayojishughulisha na uchimbaji na utafutaji madini, imezindua kampeni ya kukusanya fedha kupitia kupanda mlima Kilimanjaro, leo Jumatatu Juni 22, 2015, ambapo fedha hizo zitakwenda kusaidia sekta ya elimu kwenye maeneo yanayozunguka migodi mitatu inayomilikiwa na kampouni hiyo ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kwa safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kwenye lango la Machame,iliyo shirikisha watu 21, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Brad Gordon, alisema, kampuni yake ilianzisha mpango ujulkikanao kama “CAN EDUCATE”, ikimaanisha tunaweza kujieleimisha, imeamua kukusanya fedha kupitia kupanda mlima Kilimanjaro, ili kusaidia elimu na kampuni inimekuwa ikifanya hivyo kila mwaka.

“Lengo ni kukusanya dola za Kimarekani 200,000, zitakazosaidia jamii inayokaa kuzunguka maeneo ya migodi inayomilikiwa na kampuni hiyo” alisema Meneja Mkuu wa Uendelezaji wa Kmapuni, Asa Mwaipopo.

Posted On Tuesday, 23 June 2015 16:15

Meneja wa Airtel Money Steven Kimea (Kulia) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe itakayowazawadia wateja wa Airtel nchini kujipatia nyongeza ya Unit za bure za LUKU pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money, anayefwata kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando.Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo katika ofisi ya Airtel jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirika la umeme la (TANESCO) imezindua ofa kabambe itakayowazawadia wateja wake nchi nzima Unit za bure za Luku pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money

Ofa hii mpya ina lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme na pia kuwazawadia wateja wa Airtel wanaonunua unit za LUKU kupitia huduma ya Airtel Money

Akiongea kuhusu ofa hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackosn Mmbandoalisema” Wateja wetu watazawadia unit LUKU za ziada Bure mara tu watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money. Tunaamini ofa hii inaendana na mahitaji na mwendendo wa maisha ya watanzania. Kwa sasa manunuzi ya umeme kupitia njia nyingine si tu yanaleta changamoto za kusafiri umbali mrefu na kupoteza muda mwingi kupata huduma bali husababisha watu kukaa foleni ndefu kusubiri kununua umeme. leo Airtel tunatoa ofa hii kwa wateja wetu na kuwawezesha kununua LUKU kwa urahisi wakiwa majumbani mwao pamoja na kunawazawadia kwa kuwapatia unit za Luku za ziada za bure”.

Aliongeza kwa kusema “ Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu zinazokithi na kutatua mahitaji ya wateja wetu , tukiwa na mawakala wa Airtel Money zaidi ya 45,000 nchini , wateja wetu wanafaidika na huduma ya mikopo, huduma za kuhamisha pesa, kutoa na kuweka pesa na nyingine nyingi.

Huduma ya Airtel Timiza inayotoa mikopo isiyo na dhamana kupitia simu za mkononi ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutoa huduma za kisasa zenye ubunifu kwa watanzania.” aliongeza Mmbando

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (katikati) akiongea na waandishi wa Habari leo katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe itakayowazawadia wateja wa Airtel nchini kupata Unit za bure za LUKU pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money, kushoto ni Afisa uhusiano na matukio wa Airtel na (Kulia) Steven Kimea Meneja wa Airtel Money.(Muro)

Posted On Tuesday, 23 June 2015 16:12

Benki Kuu imekanusha vikali kwamba sarafu ya shilingi 500 ina madini ndani yake hivyo ni mali inayoweza kutumika kutengenezea vito, kufuatia uvumi potovu ulioenea kila pembe ambao unawafanya wananchi wengine wanunue sarafu hiyo kwa bei mara tano hadi kumi y thamani yake.

Akiongea na Globu ya Jamii jijini Dar es salaam leo, Meneja wa vituo vya Utunzaji wa Benki Kuu Bw. Abdul Dollah, amesema kwamba uvumi huo si kweli na kwamba katika sarafu ya shilingi 500 kuna madini machache mno ya nickel ambayo hayafai hata chembe kutengenezea vidani.

Amesema sio kweli kwamb sarafu za shilingi 500 hazipo katika mzunguko kutokana na kuhodhiwa na hao wenye kuvumisha na wanaotaka faida ya haraka haraka, na kwamba zinapatikana kwa wingi katika vituo vyake vyote.

Amesema huenda wananchi wanachanganya sarafu hiyo ya 500 na sarafu maalumu iliyotolewa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ambayo alikiri kwamba ina madini na thamani yake ni shilingi 50,000/-.(Muro)

Posted On Tuesday, 23 June 2015 15:55

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (mwenye miwani) akilakiwa na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mara, waliofika katika Ofisi ya CCM ya mkoa huo mjini Musoma Jana, kwa ajili ya kumdhamini iliaweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1,800 mkoani humo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mara, waliofika katika Ofisi ya CCM ya mkoa huo mjini Musoma Jana, kwa ajili ya kumdhamini iliaweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1,800 mkoani humo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akipongezwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Geita Juni 21.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.

Posted On Sunday, 21 June 2015 16:03

Kampuni na taasisi zinazotoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam zimeshauriwa kuanza kufikiria kuhamia katika jengo jipya la kisasa la Mamlaka ya Bandari Tanzania (kushoto) kama moja ya kuimarisha huduma za bandari.

Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Kimataifa cha Makasha (TICTS), Bw. Paul Wallace wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari katika bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. Wahariri hao walitembelea maeneo mbalimbali katika bandari hiyo.

Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga (kulia) akiwaelezea jambo wahariri wa vyombo vya habari katika bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. Wahariri hao walitembelea maeneo mbalimbali katika bandari hiyo.

Kampuni na taasisi zinazotoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam zimeshauriwa kuanza kufikiria kuhamia katika jengo jipya la kisasa la Mamlaka ya Bandari Tanzania (kushoto) kama moja ya kuimarisha huduma za bandari.

Akizungumza na timu ya wahariri waliotembelea bandari hiyo hivi karibuni, Kaimu Meneja wa bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga alisema mbali na kuwa makao makuu ya TPA, jengo hilo litakapokamilika litakuwa na kampuni na taasisi mbalimbali zinazohudumia bandari.

“Hiki kitakuwa ni kituo kimoja cha kutolea huduma za bandari...tunakaribisha maombi ya nafasi toka kwa wadau wetu mbalimbali,” alisema.

Posted On Sunday, 21 June 2015 15:56

Raia wapiga foleni kutoa fedha zao katika benki nchini Ugiriki

null

Ugiriki

Benki ya Ulaya imekubali kuidhinisha fedha zaidi za hali ya dharura kwa benki za Ugiriki.

Ombi lilitolewa baada ya watu wengi kutoa pesa nyingi kiasi kwamba jumla walizotoa zilifika yuro bilioni tatu juma hili pekee.

Wenye akaunti nchini Ugiriki wanaogopa kuwa taifa lao litachelewa kulipa madeni na pesa zao zibadilishwe kuwa sarafu za nchini badala ya Yuro yenye thamani kubwa zaidi.

Posted On Friday, 19 June 2015 16:25

Sarufi ya Tanzania

Serikali ya Tanzania inatarajia kukopa kiasi cha dola milioni mia nane za Kimarekani kutoka taasisi mbili za kifedha za kigeni ili kuimarisha shilingi ya Tanzania ambayo inaendelea kudorora.

Tayari Tanzania imefanya mazungumzo na taasisi hizo mbili ,Rand Merchant Bank ya Afrika Kusini pamoja na Benki ya Maendeleo ya China.

Benki kuu ina matumaini kwamba fedha hizo ambazo serikali ina mpango wa kukopa kwa ajili ya bajeti yake zitasaidia kuimarisha shilingi.

Posted On Thursday, 18 June 2015 18:30
Page 2 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Znateli