We have 180 guests and no members online

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali wa Dkt. Servacius Likwelile akiwa pamoja na Kamishina wa Fedha za Nje Bw. Ngosha Magonya wakati mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mjini Abidjan.

Akizungumza na vyombo vya habari mchana huu DKt.Likwelile ambaye ni amemuwakilisha Waziri wa Fedha na katika Mkutano wa Benki ya Dunia

amesema kuwa,"Mkurungezi wa Kanda ametoa ripoti ya mwaka, ameelezea ni namna gani ukanda huu wa Afrika ulivyokuwa ukifanya kazi za maendeleo, ameelezea ripoti hiyo kuwa inagusa nchi zote sita za Afrika.

Nchi hizo ni pamoja na Rwanda, Tanzania,Uganda, Kenya, Ethiophia na Visiwa vya Shelisheli, Aidha nchi hizo zimefanya kazi vizuri. Alisisitiza Likwelile.

Posted On Tuesday, 26 May 2015 05:32

DSC_0360

Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua gari la wagonjwa (Ambulance) lenye thamani ya Tsh. Milioni 80 kwa ajili ya kubebea wakinamama wajawazito na watoto wanaohitaji huduma za dharula za upasuaji kutoka vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika wilaya ya Mbogwe kwa ufadhili wa Shirika la UNFPA. Kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.

DSC_0289

Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akitoa maelezo ya mashine ya kisasa ya kuongezea damu wakina mama watakaokua wakijifungulia kwenye kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.

DSC_0062

Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla (kushoto) na Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt.Rutasha Dadi wakipitia ratiba ya sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula ambapo kitaifa yamefanyika katika Wilaya Mbogwe, Geita.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA) limekabidhi msaada wa gari la wagonjwa lenye thamani ya shilingi milioni 80 katika kituo cha afya cha Masumbwe kilichopo katika Wilaya mpya ya Mbogwe Mkoani Geita.

Shirika hilo limetoa vifaa vya kutoa huduma ya upasuaji vyenye thamani ya shilingi milioni 250 katika kituo hicho mbali na kutumia shilingi zaidi ya shilingi milioni 100 kusadia ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho.

Posted On Tuesday, 26 May 2015 04:52

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakisimama kwa heshima wakati zikipigwa nyimbo za Taifa la Tanzania na China, kwenye mapokezi yake katika Ukumbi Maalum wa Watu wa China, kwa ajili ya mazungumzo baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini Nchina.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao, wakati akikagua gwaride la heshima kwenye Ukumbi Maalum wa watu wa China, Peoples Great Hall, wakati alipofika kwa mazungumzo na mwenyeji wake baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na ujumbe wake (kushoto) akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Li Yuanchao na ujumbe wake (kulia) kwenye Ukumbi maalum wa Watu wa China, 'Peoples Great Hall' baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini China.(Muro)

Posted On Thursday, 21 May 2015 17:40

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Rukia Mtingwa akikabidhi cheti kwa Eddah Francis (kulia), mmoja wa wahitimu wa mradi wa Kuendeleza Vijana Kiuchumi Dar es Salaam katika mahafali yao yalifanyika Chuo cha ufundi stadi cha Future World, Gongo la mboto, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo. Kulia kwa Rukia ni Mkuu wa Future World, Robert Mkolla na Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter. Mradi huo umefadhiliwa na NBC kwa kushirikiana na Shirika la Plan International.

Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Rukia Mtingwa akikabidhi cheti kwa Rasuli Mikidadi (kulia), mmoja wa wahitimu wa mradi wa Kuendeleza Vijana Kiuchumi Dar es Salaam katika mahafali yao yalifanyika Chuo cha ufundi stadi cha Future World, Gongo la mboto, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam leo. Kulia kwa Rukia ni Mkuu wa Future World, Robert Mkolla na Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter. Mradi huo umefadhiliwa na NBC kwa kushirikiana na Shirika la Plan International.(Muro)

Posted On Wednesday, 20 May 2015 05:30

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameyataka makampuni yanayojihusisha na mafuta na gesi nchini, kuhakikisha yanatimiza mahitaji ya Soko la Ndani na ukanda wa Afrika Mashariki kabla ya kufikia Soko la Nje.

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Utafiti na ufunguzi wa kozi ya Shahada ya Uzamili ya Mafuta na Gesi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika hotuba iliyosomwa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alisema Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki bado una mahitaji makubwa ya rasilimali ya gesi hususani katika viwanda na nyanja zote.

Posted On Tuesday, 19 May 2015 06:10

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani.

KUKOSEKANA kwa Sheria ya kutenganisha biashara na uongozi ili kuweka nidhamu kwa viongozi wa umma kumesababisha kuwepo na mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa viongozi hao, ambao wamekuwa wakitumia ofisi za umma kwa maslahi binafsi, hivyo kufanya vitendo vya rushwa kukithiri.

Wakichangia mjadala wa hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma bungeni jana, wabunge mbalimbali walisema ukosefu wa sheria hiyo umesababisha kuwepo kwa mianya mingi ya rushwa inayofanywa na baadhi ya watumishi wa umma.

Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Manyoni Mashariki, John Chiligati (CCM) alisema hivi sasa kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili na baadhi ya viongozi wa umma hutumia ofisi za umma kwa maslahi binafsi.

Posted On Tuesday, 19 May 2015 06:04

Muonekano wa jengo la Tropical Centre barabara ya Bagamoyo maeneo ya Victoria jijini Dar es salaam ambapo kituo cha AAR Healthcare kinapatikana hivi sasa katika ghorofa ya pili.

Sehemu za ndani za kituo kipya cha AAR

Kituo maarufu cha afya cha AAR Healthcare sasa kimehamia ghorofa ya pili katika jengo la Tropical Centre lililopo barabara ya New Bagamoyo road na Uporoto Street maeneo ya Victoria jijini Dar es salaam, kutoka mtaa wa Chato, na kinaendelea kutoa huduma zake bora kwa wananchi katika mazingira ya kisasa zaidi kila siku kwa kuanzia saa moja unusu asubuhi hadi saa mbili usiku.(Muro)

Posted On Tuesday, 19 May 2015 06:01

Sehemu ya Wawakilishi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa katika siku yao ya kwanza ya mkutano wa siku nne unaojadili juu ya mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Maendeleo Endelevu ya Maendeleo baada ya 2015. Majadiliano hayo ni moja ya eneo muhimu kueleleka ukamilishaji wa Mchakato wa Ajenda na Malengo SDGs. Mkutano huu unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Afisa Mkuu wa uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bw. Songelael Shilla, akizungumza wakati wa Mkutano wa pembezoni ( Side-Event) ulioandaliwa kwa ushirikiano kati ya Uwakilishi na Asasi za Kimataifa, kwaajili ya kubadilishana mawazo kuhusu nafasi za Ki Kanda na Kitaifa katika mfumo wa ufuatiliaji na udhibiti, fursa na changamoto za Malengo ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015 kwa upande wa Afrika.

Sehemu wa Washiriki wa mkutano huo wa pembezoni ambapo washiriki pamoja na mambo mengine walisisitiza haja na umuhimu wa wananchi kushirikishwa kikamilifu katika eneo hilo la ufanyaji wa tathmini na ufuatiliaji kwa kile walichosema malengo hayo ya maendeleo endelevu yanawahusu wananchi hiyo ushiriki wako ni muhimu.

Posted On Tuesday, 19 May 2015 05:52

Mkurungezi wa Utafiti Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. Emma Msaky, akizungumza na wataalam wanao endelea na uchimbaji wa visima vifupi katika Mradi Ujulikanao kama MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT kwa ajili wa utafiti wa mafuta na gesi kijiji cha Jihirini, wilayni Mkinga mkoani Tanga.

Mkurungezi wa Utafiti Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. Emma Msaky, akionyesha sampuli za utafiti mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Mradi wa utafiti wa mafuta na gesi Ujulikanao kama MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT kijiji cha Jihirini, wilayni Mkinga mkoani Tanga.

Meneja wa Mradi wa MP 10 GOMBERO DRILLING PROJECT, Dkt. Amina Karega, akionyesha sampuli za utafiti mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kijiji cha Jihirini, wilayni Mkinga mkoani Tanga.

Na. Augustino Kasale - Kitengo Cha Mawasiliano-TPDC

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania limeanza utafiti wa mafuta na gesi eneo la Gombero, Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga.

Mkurugezi wa Utafiti kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Dkt. Emma Msaky, mwishoni mwa wiki alitembelea kujionea shughuli inayo fanya na Shirika hilo.

Posted On Monday, 18 May 2015 18:27

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya maandalizi ya Maonyesho ya Biashara ya China 'Expo Central China 2015', wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Mikutano wa 'Wuhan International Exhibition Centre VVIP Room'. Mkutano huo umeanza leo Mei 18 2015 jijini Wuhan, Jiombo la Hubei.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi wa nchini China, Katibu wa Chama Tawala cha CPC cha Nchini China, Jimbo la Hubei, Li Hongzhong (kushoto) na wengine, wakati alipofungua Maonesho ya Biashara ya China 'Expo Central China 2015', yaliyoanza leo Mei 18, 2015, Jimbo la Hubei, Jijini Wuhan nchini China.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na Katibu wa Chama Tawala cha CPC cha Nchini China, Jimbo la Hubei, Li Hongzhong (kushoto) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya China 'Expo Central China 2015'.

Posted On Monday, 18 May 2015 18:04

Displaying 01.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Edward Marks (kushoto), akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) , Rished Bade (kulia) katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake, baadhi ya wafanyabiashara na watendaji kutoka taasisi mbalimbali ili kufahamiana. Hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Ofisa Fedha Mkuu wa NBC, Jaffari Matundu.

Displaying 02.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Edward Marks (wa pili kulia), akizungumza na baadhi ya wateja pamoja na maofisa wa benki hiyo katika hafla iliyoandaliwa na NBC kwa ajili ya wateja wake, baadhi ya wafanyabiashara na watendaji kutoka taasisi mbalimbali ili kufahamiana. Hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Displaying 03.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Edward Marks (katikati), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Chemi Cotex, Lakshmi Narayan Rathi (kulia) katika hafla iliyoandaliwa na NBC kwa ajili ya wateja wake, baadhi ya wafanyabiashara na watendaji kutoka taasisi mbalimbali ili kufahamiana. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Fedha Mkuu wa NBC, Jaffari Matundu.

Posted On Monday, 18 May 2015 04:56

Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Martin Mmari, (kushoto), akimkabidhi cheti Mfanyakazi bora wa Mfuko huo kutoka kanda ya Ziwa, Bernard Kyaduma, wakati wa hafla ya kuwapatia tuzo wafanyakazi bora wa Mfuko huo mwaka 2014.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Julius Kam Mganga, (wapili kushoto), akitunuku cheti Mfanyakazi bora wa jumla wa Mfuko huo kwa mwaka 2014, Angelina Napacho kutoka kurugenzi ya Operesheni ya Mfuko huo, wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi bora kutoka kila idara kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumapili Mei 17, 2015. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa ndani, Hoseah Kashimba, na Mkurugenzi wa Fedha, Martin Mmari.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Julius Kam Mganga, akitoa hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, William Erio.

Posted On Sunday, 17 May 2015 16:39
Page 4 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Maji