We have 142 guests and no members online

001.MAHELA fe923

Meneja wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Bw.Benjamin Michael akiongea kwenye simu na mmoja wa washindi aliejishindia shilingi Milioni 5 katika  Promosheni ya"MAHELA"inayoendeshwa na kampuni hiyo,katikati Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu na Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini  Bw. Abdallah Hemedy,ambapo wakazi ya jijini Dar es Salaam Bw.Ramadhan Kibanike(62)na Bi.Maselina Apolinali wamejinyakulia kitita cha shilingi Milioni tano tano kila mmoja.Zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa.

002.MAHELA 84ae0

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu (katikati)akiwasiliana na Bi.Maselina Apolina,mkazi wa jijini Dar es Salaam ukonga magereza alieibuka mshindi wa kitita cha shilingi Milioni tano katika Promosheni ya"MAHELA"inayoendelea kuchezeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom,zaidi ya shilingi Milioni 400 zinaendelea kushindaniwa,wanaoshuhudia kushoto ni Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,Bw.Benjamin Michaelna kulia ni Msimamizi wa Michezo ya kubahatisha nchini Abdallah Hemedy.

Posted On Tuesday, 05 March 2013 11:11

1. Kadamnasi ikimsikiliza Waziri© 2013 Urban Pulse Creative_96
Kadamnasi ikimsikiliza Waziri kwa makini, ukumbi wa Ubalozi wetu London.Wapo waliokuja kuuliza maswali. Au waliotaka tu kufahamishwa. Wapo waliojaribu kumbana Waziri wakijibishana naye masuala ya kisiasa. Wote walipewa nafasi katika hizo saa nne. Muhimu ilikua kuithamini nchi yako.

Posted On Tuesday, 05 March 2013 06:14

Photo: Uchambuzi: Tunajifunza Nini Kutoka Kenya?
Ndugu zangu,
AFRIKA vurugu zetu nyingi zinaanzia kwenye chaguzi. Joseph Stalin wa Urusi aliwahi kutamka: "Anayepiga kura hana anachoamua, anayehesabu kura ndiye anayeamua kila kitu". 
Na hapa ndipo lilipo tatizo la msingi. Watu kukosa imani na wenye kusimamia uhesabuji wa kura zenyewe. Kuna wanaojisikia kuwa kura zao hazina umuhimu; kwani, mwisho wa yote, kura zitaibwa. 
Katika nchi zetu hizi, kukosa imani na wenye kusimamia mchakato wa uchaguzi hadi kuhesabu kura ndio chanzo cha vurugu na uvunjifu wa amani. Tuliyaona hayo kwa jirani zetu kule Kenya mwaka 2007.
Wakenya wale walishiriki mchakato wa kujiandikisha na hata kupiga kura bila matatizo makubwa. Kazi ikaja kwenye kuhesabu kura. Ndipo hapo hesabu zikaanza kuwa ngumu. Kukawa na kufuta hapa na pale. Kukawa na kushinikizana matokeo na kadhalika. Hatimaye damu ikamwagika. 
Kila mwenye kufikiri alielewa kuwa kiini cha vurugu za Kenya ni Tume ya Uchaguzi ambayo haikuwa huru. Wakenya wale wakajifunza. Leo wana Katiba mpya. Katiba ya watu wa Kenya. 
Hivyo basi, tunachojifunza hapa ni kuwa, dawa ya kuepuka au kupunguza shari kama iliyotokea Kenya ni kwa nchi zetu hizi kuangalia upya Katiba zetu hizi na hususan inapohusu uchaguzi na Tume ya Uchaguzi. Na kikubwa kinachosababisha vurugu na watu kuchinjana ni kukosekana kwa imani kwa wenye kusimamia uchaguzi. 
Hapa kwetu tuliyaona hata kwenye Uchaguzi mdogo wa kule Arumeru. Mliokuwa kwenye runinga mkiangalia usiku ule wa uchaguzi na kusubiri matokeo mtakuwa mlikiona pia nilichokiona mimi.
Hakika niliogopa, kwamba televisheni inatumika kuendesha propaganda za kuwaonyesha vijana kuwa ni wenye vurugu wakati hatuonyeshwi vijana hao wakifanya vurugu.
 Mtangazaji mmoja alipokuwa hewani moja kwa moja cha kwanza kutuambia ni : " Kuna milio ya risasi inasikika" bila kutuacha watazamaji tuisikie pia hiyo milio ya risasi.
Ndio, kule Arumeru tumeona jinsi baadhi ya vyombo vya habari na wanahabari wakishiriki kusambaza hofu ya vijana kufanya vurugu bila kutuonyesha vijana wanaofanya vurugu. Bila wanahabari hao kutambua au labda walitambua wangeweza kabisa kuwa chanzo cha vurugu na hata mauaji.
Jirani zetu Kenya wameshajifunza kutokana na maafa ya uchaguzi wa 2007 yaliyolifika taifa hilo. Na Wakenya wamegundua, kuwa si tu Polisi wanaoweza kuchochea vurugu na mauaji, bali hata wanahabari kama ilivyokuwa mwaka 2007. Ndio maana, kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa siku hii ya leo, Wakenya walishaamua, tangu mwaka jana, kuendesha mafunzo maalumu kwa wanahabari watakaoripoti habari za uchaguzi mkuu. Lengo kuu hapo ni kuwafanya wanahabari hao wasijikite kuandika habari za uchochezi na zilizoegemea kwenye vyama na makundi. Ni hatua sahihi na ya kuigwa.
Na matokeo ya Uchaguzi wa Kenya yatakuwa kama ‘ litmus paper’- ni kipimo watakachotumia wakubwa katika mahusiano yao na nchi zetu hizi. Kama Wakenya watafanya uchaguzi wao kwa amani na matokeo yakatangazwa na Tume Huru, Rais akaapishwa na shughuli zikaendelea, basi, huenda matokeo hayo yakaifanya Kenya kuwa ‘ Kaka Mkubwa’ kwa nchi zetu hizi za Afrika Mashariki na Kati. Tutakuwa ni watu wa kuambiwa; “ Waangalieni wenzenu Wakenya!”
Kila la Kheri Jirani zetu wa Kenya.
Maggid,
Msamvu, Morogoro.

 

Ndugu zangu,

AFRIKA vurugu zetu nyingi zinaanzia kwenye chaguzi. Joseph Stalin wa Urusi aliwahi kutamka: "Anayepiga kura hana anachoamua, anayehesabu kura ndiye anayeamua kila kitu".

Na hapa ndipo lilipo tatizo la msingi. Watu kukosa imani na wenye kusimamia uhesabuji wa kura zenyewe. Kuna wanaojisikia kuwa kura zao hazina umuhimu; kwani, mwisho wa yote, kura zitaibwa.

Katika nchi zetu hizi, kukosa imani na wenye kusimamia mchakato wa uchaguzi hadi kuhesabu kura ndio chanzo cha vurugu na uvunjifu wa amani. Tuliyaona hayo kwa jirani zetu kule Kenya mwaka 2007.

Posted On Monday, 04 March 2013 16:16

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), SteveKilindo (katikati), akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Ibrahim Msengi  msaada wa magodoro kwa ajili ya Hosptali ya Huruma ya wilayani Rombo pamoja na Kituo cha Afya cha Uru Kiaseni katika hafla iliyofanyika Mjini Moshi. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa mkoa huo, Dk. Mtumwa Mwako. Jumla ya magodoro 210 na vyandarua 200 vimetolewa na TBL kwa ajili ya kituo hicho na hospitali hiyo.

 

Posted On Sunday, 03 March 2013 14:25

i 001 126f5

Posted On Sunday, 03 March 2013 06:37

 Rais wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya ISACA Tawi la Tanzania, Boniface Kanemba akifafanua jambo wakati wa semina kuhusu teknolojia ya mawasiliano na Utawala Bora vinavyoweza kuchangia maendeleo ya uchumi na kufanyika jijini Dar es Salaam. Semina hiyo iliandaliwa na ISACA Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Norway Registers Development. (Picha na Habari Mseto Blog)

Posted On Saturday, 02 March 2013 16:55

000000000000000000000000 81235

WAZEE WA KAZI

  CONTAINER PRICE CUT!

40'HC TO DAR/MOMBASA NOW £1,950

20' CONTAINER TO DAR/MOMBASA £1,350

THIS IS MORE THAN £300 DISCOUNT!

THIS IS FOR MAERSK LINE, CMA-CGM, WEC LINE NA SAFMARINE

 

RATIBA YA MELI MPYA FEBRUARY 2013

Posted On Saturday, 02 March 2013 16:20

0000000xx00000 c5a03

Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Theresia Mahongo akizungumza na mjasiriamali ambaye ni mlemavu Mariam Said katikati baada ya kumaliza kuongea na wajasiriamali katika ukumbi wa veta iringa. kulia ni mkurugenzi wa veta nyanda za juu Monica Mbelle, afisa mikopo wa sido neserian Laizer na kaimu mkuu wa chuo cha veta charles  kimbira.

Posted On Saturday, 02 March 2013 09:29

Photo: Neno La Leo: Mengine Tuyafanyayo Hupelekea Maanguko Yetu!
Ndugu zangu, 
Kupitia kitabu chake ’ Kusadikika’, mwanafasihi Shaaban Robert anamwelezea mchwa anayekaribia kufa.
Kwamba huota mbawa. Hukiacha kichuguu . Yumkini ataruka juu sana. Atakwenda mbali. Lakini, huko angani hufika mahali, mbawa hupukutika. Mchwa ataanguka chini. Mbali na kichuguu.
Hapo, mchwa hukabiriwa na hatari kubwa. Hawezi kuruka tena, na yu mbali na kichuguu. Na kichuguu ni taasisi. Hivyo, mchwa anaweza kuliwa na kinyonga, au hata chura. Na akinusurika na wawili hao, aweza kukanyagwa na unyayo wa mwanadamu, au hata tairi la baiskeli. Mchwa atakufa.
Naam, mengine tuyafanyayo hupelekea maanguko yetu. Hata kama mwanzoni huonekana kutupaisha juu angani.
” Nafikiri, ndio maana naishi”- Anasema mwanafalsafa Rene Descartes.
Na maarifa ya Sayansi yanatusaidia kuyabaini mahusiano kati ya dunia tunayoishi na mazingira yanayotuzunguka. Hiyo ni falsafa ya kivitendo. Ndio iliyo bora kuliko ile dhanifu- Speculative.
Iweje basi tumekuwa ni watu wa kuishi kwa dhahnia na hata kusambaza uvumi?
Tusisahau, kuwa kiu ya mwanadamu siku zote ni kutaka kuujua ukweli. Ukweli mzima.
Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
<a href=
Ndugu zangu,

Kupitia kitabu chake ’ Kusadikika’, mwanafasihi Shaaban Robert anamwelezea mchwa anayekaribia kufa.

Kwamba huota mbawa. Hukiacha kichuguu . Yumkini ataruka juu sana. Atakwenda mbali. Lakini, huko angani hufika mahali, mbawa hupukutika. Mchwa ataanguka chini. Mbali na kichuguu.

Hapo, mchwa hukabiriwa na hatari kubwa. Hawezi kuruka tena, na yu mbali na kichuguu. Na kichuguu ni taasisi. Hivyo, mchwa anaweza kuliwa na kinyonga, au hata chura. Na akinusurika na wawili hao, aweza kukanyagwa na unyayo wa mwanadamu, au hata tairi la baiskeli. Mchwa atakufa.

Posted On Friday, 01 March 2013 14:17

Vinauzwa Kigamboni eneo la potea unapita njia ya kuelekea Dar zoo viwanja vimepimwa, Viwanja hivi havipo kwenye eneo la mradi wa makazi ya mji mpya wa kigamboni hivyo usiwe na shaka.  viwanja vinafaa kwa matumizi ya ujenzi wa makazi au  Hotel.

land c1f1c

Mawasiliano # 0766974242 au 0655227507 . Email mwipopo@gmail.com

Posted On Friday, 01 March 2013 06:24

Photo: Neno Fupi La Usiku Huu: Elimu
Ndugu zangu,
Napenda usiku huu nitaje matatu tu miongoni mwa ninayoamini kuwa ni malengo ya nchi kwenye elimu ;
- Kuimarisha Umoja wa Kitaifa na kupunguza pengo la walio na wasio nacho.
-Kuwaendeleza walioelimika kuwa raia wema.
-Kuendeleza uchumi wa nchi.
Na elimu ni nini hasa? 
Jibu; ni shughuli yenye maana na tija kwa anayeifanya. Ni sharti iwe na dhumuni na malengo. 
Ndio, ni shughuli muhimu sana kwa mwananamu na nchi. Na kwa nchi,  ni shughuli yenye gharama.
Na hakuna nchi yeyote duniani iliyopiga hatua za maana kwenye kinachoitwa maendeleo bila kuwekeza kwa wingi kwenye elimu. Hivyo, elimu ndicho kitu cha kwanza.
Na hilo ni Neno Fupi la Usiku Huu.
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
<a href=
Ndugu zangu,
Napenda usiku huu nitaje matatu tu miongoni mwa ninayoamini kuwa ni malengo ya nchi kwenye elimu ;
- Kuimarisha Umoja wa Kitaifa na kupunguza pengo la walio na wasio nacho.
-Kuwaendeleza walioelimika kuwa raia wema.
-Kuendeleza uchumi wa nchi.

Posted On Friday, 01 March 2013 03:31

 Makao makuu ya Kampuni ya BG.

 Mh waziri  Muhongo akisalimia na CEO wa BG Chris.

Posted On Thursday, 28 February 2013 13:50
Page 40 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart