We have 82 guests and no members online

Meneja Bidhaa wa Benki Ya Exim Tanzania, Aloyse Maro (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kutangaza uzinduzi wa kampeni mpya ya benki hiyo inayolenga kuhamasisha wateja juu ya matumizi ya kadi mpya ya Faida Debit Card, ambayo imeimarishwa zaidi kiusalama, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko Msaidizi wa benki hiyo, Anita Goshashy (kushoto) na Zawadi Kanyawana kutoka kitengo cha Huduma za Rejareja za Kibenki (katikati)

Meneja Bidhaa wa Benki Ya Exim Tanzania, Aloyse Maro (katikati)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kutangaza uzinduzi wa kampeni mpya ya benki hiyo inayolenga kuhamasisha wateja juu ya matumizi ya kadi mpya ya Faida Debit Card, ambayo imeimarishwa zaidi kiusalama, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko Msaidizi wa benki hiyo, Anita Goshashy (kushoto) na Zawadi Kanyawana kutoka kitengo cha Huduma za Rejareja za Kibenki (kulia).

BENKI ya EximTanzania imezindua kampeni inayolenga kuwahamasisha wateja wake juu ya matumizi ya kadi zake mpya za 'Faida Chip and PIN Debit card' ambazo zimeundwa kwa kuzingatia vigezo vya kiusalama zaidi.

Kwa mujibu wa Meneja Bidhaa wa benki hiyo Bw. Aloyce Maro hatua hiyo ni sehemu ya jitiahada za benki hiyo kuhakikisha kwamba huduma zake zinatolewa kwa uhakika na usalama zaidi kwa faida ya wateja wake.

Posted On Tuesday, 12 May 2015 07:21

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Ngula Cheyo, katikati akizungumza jambo wakati wa droo ya pili ya Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ambapo jumla ya washindi watatu kila mwezi wanapatikana na kila mmoja kujishindia jumla ya Sh Milioni moja. Kulia ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa taasisi hiyo, Gladys John, huku kushoto akiwa ni bwana Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania. Picha zote na Mpiga Picha wetu.

Afisa wa Huduma kwa Wateja wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Gladys John katikati akichagua koponi ya mmoja wa washindi wa shindano la Kopa Bayport linaloendelea ambapo washindi watatu wamepatikana na kila mmoja kupata bahati ya kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz. Kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, wakati kushoto ni Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Posted On Saturday, 09 May 2015 17:24

kwana

Bodi ya UTT-PID ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. E Mlaki pamoja na Menejimenti wakiwa na wenyeji wao katika jiji la Chengdu ambapo walifanya ziara katika maeneo tofauti ya uwekezaji na manufaa wanayopata wananchi wa jiji hilo. Ziara hiyo ya siku Tano katika Miji tofauti inatarajia kukamilika Tarehe kumi kabla ya kurejea nyumbani.

pili

Bodi ya UTT-PID pamoja na Menejimenti ikipata Maelezo kutoka wataalum wa uzalishaji nishati toka mji wa Chengdu.

Na Mwandishi Maalum

Bodi ya Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyo chini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID), pamoja na Menejimenti yake ipo nchini China katika ziara maalum ya Mafunzo na kujenga uzoefu ya siku tano ikiwa na lengo la kuimmalisha utendaji kaziw wa taasisi hiyo.

Katika ziara hiyo, Bodi ya UTT-PID, ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. E Mlaki pamoja na Menejimenti wapo katika miji mbalimbali na kutembelea maeneo tofauti ya uwekezaji ilikushuhudia manufaa wanayopata wananchi wa maeneo hayo.

Kazi za UTT-PID ni pamoja na Utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.(Muro)

Posted On Saturday, 09 May 2015 17:22

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akihojiwa na Priscilla Lecomte wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa. (Picha: UN/JosephMsami)

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa jopo la Umoja wa Mataifa la kusaka jinsi dunia inaweza kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kwa siku za usoni, amesema leo kwamba anatarajia kutoa mapendekezo juu ya mapugunfu yaliyoonekana wakati wa kupambana na Ebola.

Akihojiwa na Priscilla Lecomte na Jospeh Msami wa idhaa hii, ameeleza kwamba wanachama wa jopo hilo baada ya kuzungumza na wataalam wa afya mjini new York, watatembelea Geneva, Uswisi, ili kujadiliana na wadau wa shirika la afya ulimwenguni, WHO na mashirika mengine, halikadhalika watasafiri kwenda nchi zilizoathirika na Ebola.

Hapa Rais Kikwete anaanza kwa kuelezea jukumu la jopo hilo ambalo ripoti yake ya awali wataiwasilisha mwezi Septemba, ripoti ya mwisho ikitarajiwa mwisho wa mwaka .

KUSIKILIZA BONYEZA HAPA

http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/2015/05/rais-kikwete-atumaini-kuvumbua-jinsi-ya-kuimarisha-utayari-wa-jamii-dhidi-ya-majanga-ya-afya(Muro)

Posted On Saturday, 09 May 2015 14:17

Mkurugezi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifungua semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB katika ukumbi wa AICCjijini Arusha leo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza wakati wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB.

Mwanahisa akiuliza swali.(Muro)

Posted On Saturday, 09 May 2015 05:51

Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Jinsia na watoto akizungumza na Wajasialiamali mbalimbali kuhusiana na kujiinua kiuchumi katika ukumbi wa JB belomente jijiji Dar es Salaam leo.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Jinsia na Watoto Anna Kilango akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Bodi ya wanawake wafanyabiashara Tanzania Anna Matinde katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa JB Belomente jijiji Dar es Salaam leo kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya Equity Josef Iha.

Baadhi ya wajasiliamali waliohudhuria katika warsha iliyofanyika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa JB Belomente jijiji Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakaingo, blobu ya Jamii.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

WANAWAKE wametakiwa kujiunga katika taasisi za fedha ambazo zinaainisha mikopo ya wajasiriamali hiyo itasaidia wanawake kujikwamua na umasikini.

Hayo ameyasema leo Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Sophia Simba wakati wa uzinduzi wa mpango Fanikisha Plus wa wajasirimali unaondeshwa na benki ya Equity iliyofanyika leo katika ukumbi JB,Belmote jijini Dar es Salaam.

Posted On Saturday, 09 May 2015 05:42

Viongozi wa Chadema wakiomba dua kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika Dar es Salaam jana. Kuanzia kulia ni Makamu Mwenyekiti, Profesa Abdallah Safari, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu. Picha na Venance Nestory

Dar es Salaam. Kamati Kuu ya Chadema imepanga Agosti 4 kuwa siku ya kumpata mgombea wake wa urais ambaye ataingia kwenye kinyang'anyiro cha kumtafuta mgombea wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Vyama vinne vilivyounda Ukawa, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, vimekubaliana kusimamisha mgombea mmoja wa kuanzia ngazi ya urais, lakini kila chama kitateua mgombea wake kabla ya kukubaliana mtu atakayeungwa mkono na vyama vyote.

Ratiba iliyotolewa jana na Chadema inaonyesha kuwa chama hicho kitatumia siku 76, kuanzia Mei 18, kumaliza mchakato wa kuwapata wagombea wake wa nafasi za udiwani, ubunge na urais kwa kuhitimisha na Mkutano Mkuu. Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Chadema itampata mgombea wake wa urais takriban siku 14 zaidi kulinganisha na mwaka 2010 wakati Dk Willibrod Slaa alipoteuliwa.

Kwa mujibu wa Ibara ya 7.710 (C) ya katiba ya Chadema, Mkutano Mkuu ndiyo chombo chenye mamlaka ya kumpitisha mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho.

Posted On Wednesday, 06 May 2015 06:07

Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akielekeza jambo wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine amesifu kasi ya ujezi wa nyumba hizo unaozingatia viwango na muda na akawataka wafanyakazi wa NHC kuchapa kazi ili kufikia malengo yao waliyojiwekea. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa NHC, Felix Maagi, wa pili ni Eliaisa Keenja wa NHC, Meneja wa NHC mkoa wa Mtwara, Joseph John na Injinia wa mradi huo Leonard Kazoba.

Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akimsikiliza Mhandisi wa mradi huo Leonard Kazoba wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara.

Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Mchumo akimsikiliza Mhandisi wa mradi huo Leonard Kazoba wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye mradi wa nyumba za gharama nafuu Masasi, mkoani Mtwara.

Posted On Monday, 04 May 2015 04:24

Mhandisi wa Sunnrgy,Erick Mhema akielezea wadau mbalimbali kifaa cha kuvuta maji kutokana na kutumia Nishati ya jua (Solar Energy),wakati wa mkutano wa Wadau wa Nishati ya Jua na Upepo iliyofanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Kamishina wa Nishati na Petroli wa Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Hosea Mbise akizungumza na waandishi na vyombo vya habari katika mkutano wa Wadau wa Nishati ya Jua na Upepo iliyofanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Mhandisi wa Sunnrgy,Erick Mhema akizungumza na waandishi na vyombo vya habari katika mkutano wa Wadau wa Nishati ya Jua na Upepo iliyofanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Posted On Thursday, 30 April 2015 17:02

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) nchini Tanzania Dkt.Albina Chuwa akifungua Kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala la wataalam na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam. Kongamano hilo la siku 2 linajadili namna Bora ya uendeshaji wa Taasisi za Takwimu na namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za masuala ya Takwimu Barani Afrika.

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Takwimu ya Bara la Afrika Bw. Joseph ILboudo akizungumza na watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu Kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala lililowahusisha wataalam na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam.

Bw. Andry Andriantseheno kutoka UNECA akiongoza kongamano hilo la siku 2 la watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu wa nchi za Afrika linalojadili masuala ya Uongozi na utawala na leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Tanzania wenyeji wa mkutano huo.

Posted On Thursday, 30 April 2015 16:45

Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli akizungumza katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi wa wizara Ujenzi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.

 Mhandisi Mussa Lyombe akizungumza leo jijini Dar es Salaam,katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya ujenzi.

 Baraza la wafanyakazi wa wizara ya ujenzi waliohudhuria katika ufunguzi wa baraza hizo leo jijini Dar es Salaam.

Posted On Thursday, 30 April 2015 16:19

 Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum.

SERIKALI imewasilisha mwelekeo wa bajeti kwa Kamati ya Bunge, ambayo inalenga zaidi kupeleka umeme na huduma za maji vijijini, kumalizia miradi ambayo haijakamilika na kutenga fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.

Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisema wanaandaa bajeti ambayo itasaidia kumaliza mambo yote waliyoahidi, ambayo yameainishwa kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambayo serikali iliahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.

"Bajeti ya mwaka 2015/16 ni ya kipekee. Ni mwaka wa uchaguzi, ni mwaka ambao serikali ya Awamu ya Nne inamaliza muda wake na serikali mpya kuingia madarakani. "Ni mwaka ambao Mkukuta na Mpango wa Kwanza wa Maendeleo ya Milenia ya miaka mitano inafikia tamati, Malengo ya Milenia ya mwaka 2015 yanafikia ukomo na pia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2010 unakamilika," alisema.

Posted On Thursday, 30 April 2015 06:07
Page 5 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu