We have 365 guests and no members online

pedre 65d50

Padre Ambrose,aliyepigwa risasi hivi karibuni

One Does Not Kill A Priest, Not A Sheikh Either!


Ndugu zangu,
Nimepokea kwa masikitiko makubwa habari za kuuawa kwa Padri Mushi wa Kanisa la Minara Miwili huko Zanzibar asubuhi ya leo.

Tumelelewa tukiamini, kuwa hakuna atakayethubutu kumpiga risasi Padri au Sheikh.

Posted On Sunday, 17 February 2013 10:24

Christine Mhando 7315c

Na Freddy Macha

Maonyesho maarufu ya mavazi ya kimataifa –London Fashion Week- yatamega kitengo chake
cha kimataifa kusaidia kutangaza kazi za washoni wapya toka Tanzania ndani ya Ubalozi wetu
leo Ijumaa mjini London.

Mada ya maonyesho haya yatakayoendelea kwa juma zima ni “Swahili Flavour” (Ladha ya
Kiswahili). Yametayarishwa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania London na Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) kujenga vipaji na kazi za mavazi za washoni wasiofahamika duniani.

Posted On Friday, 15 February 2013 11:56

Na: Frederick Katulanda, Mwanza- Mwananchi

JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa kusaidiana na maofisa wa Benki ya NMB imewatia mbaroni watu watatu ambao wanadaiwa kuiba kiasi cha Sh700 milioni kwa nyakati tofauti. Watuhumiwa hao wamenaswa baada ya kuwekewa mtego na maofisa wa benki na polisi kwenye saa 6.00 usiku wa Februari 10, mwaka huu na mtuhumiwa mmoja alibambwa akichukua fedha katika ATM ya NMB kwenye Tawi la PPF Plaza Mwanza. Baada ya kunaswa kwa mtuhumiwa huyo,

Posted On Friday, 15 February 2013 09:46

 

ndc

Dk Anacleti Kashuliza Katibu Mtendaji wa  Baraza la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi  NCC akibadilishana mikataba wa ushirikiano kuwawezesha wananchi na Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji  wa Shirika la Maendeleo la Taifa NDC Bw. Shannel Mvungi           

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) wameanzisha ushirikiano utakaowawezesha wananchi kiuchumi katika maeneo ambayo NDC imeanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo. Manufaa haya kwa wananchi yanatokana na kusainiwa kwa Makubaliano ya ushirikiano kati ya mashirika haya ambao unalenga kutoa fursa kubwa za ushiriki wa kiuchumi kwa wananchi wa maeneo husika.Hadi sasa,

Posted On Friday, 15 February 2013 09:19

Photo: Neno Fupi La Usiku Huu: Ukimya Wa Marafiki Unaumiza Zaidi Kuliko Kelele Za Maadui...!
Ndugu zangu, 
Maneno hayo juu yalipatwa kutamkwa na  Martin Luther King ( Jr) alipokuwa gerezani.
Mwanadamu unapokuwa kwenye matatizo unawahitaji zaidi wanadamu wenzako, na hususan marafiki.
Moja ya hotuba bora kabisa kupatwa kutolewa na Julius Nyerere ni ile ya mwezi Oktoba mwaka 1978. Ni pale alipotangaza vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda. 
Nilikuwa na miaka 12 tu. Nakumbuka niliisikiliza hotuba ile kutoka mwanzo hadi mwisho; neno kwa neno.  Nikiri, kuwa Julius Nyerere alikuwa hodari sana kwenye rhetoric- sanaa ya kuzungumza.
Kwa mtawala, kuamrisha vikosi vya nchi yako kwenda vitani ni moja ya maamuzi magumu sana. Na wakati mwingine, hotuba ya kuamrisha vita yaweza kuamua hatma ya vita. 
Kwenye hotuba ile, Julius Nyerere  aliweka vema msingi wa hoja, ya kwanini, sisi , kama taifa, tulilazimika kwenda vitani.
Na akatamka yafuatayo yaliyosisimua na kuhamasisha vikosi na taifa kwa ujumla. Kwamba;
- Uwezo wa kumpiga Amin tunao...
- Sababu ya kumpiga Amin tunayo..
- Na nia ya kumpiga Amin tunayo...
Kisha akatoka nje ya mipaka yetu akitamka; 
" Tunataka dunia ituelewe hivyo". Akaonyesha pia kuwa taifa lina marafiki kwa kutamka;
" Marafiki zetu kwanza tuacheni, tumwonyeshe mshenzi huyu!"
Naam, katika maisha, mwanadamu kuna wakati unalazimika kuingia vitani. Unalazimika kupambana kudai haki yako na kulinda hadhi yako.  Hayo ni mapambano ya haki. Na vita ya kudai haki ni vita ya lazima kupiganwa.
Hapo mwanadamu anakuwa kwenye matatizo. Katika hali hiyo, anachohitaji mwanadamu ni kuungwa mkono na marafiki zake. 
Katika hilo, kama alivyotamka Martini Luther King Jr, kwamba ukimya wa marafiki unaumiza zaidi kuliko kelele za maadui.
Na hilo ni Neno Fupi la Usiku Huu.
Maggid Mjengwa,
Iringa.


Ndugu zangu,

Maneno hayo juu yalipatwa kutamkwa na Martin Luther King ( Jr) alipokuwa gerezani.

Mwanadamu unapokuwa kwenye matatizo unawahitaji zaidi wanadamu wenzako, na hususan marafiki.

Moja ya hotuba bora kabisa kupatwa kutolewa na Julius Nyerere ni ile ya mwezi Oktoba mwaka 1978. Ni pale alipotangaza vita dhidi ya mvamizi Idi Amin wa Uganda. 

Posted On Friday, 15 February 2013 08:49

 

 

3

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiwa anakata utepe wa lango la kuingia katika ukumbi wa World Garden uliozinduliwa leo jijini Arusha.
1

Ukumbi wa World Garden unavyoonekana kwa mbele.

2

Mkuu wa mkoa wa Arusha akiwa na wageni waalikwa wakitembelea ukumbi wa disco wa World Garden mara baada ya kuuzindua.

 

Na: Woinde Shizza ,Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kuanza kuwekeza katika sekta mbalimbali ili kuweza kuweka mkoa huo katika madhari  na hadhi ya jiji. Aliyasema hayo jana wakati akifungua jengo jipya la mikutano pamoja na ukumbi wa disco lililopo jijini hapa lijulikanalo kwa jina la World garden lililopo katika kata ya

Posted On Thursday, 14 February 2013 14:51

Mkurugenzi Mtendaji Ecobank Enoch Osei-Safo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa halfa fupi ya kukabidhi zawadi ya gari mpya aina ya  Hyundai Tucson ix35 kwa mshindi wa Shindano lililokuwa likiendeshwa na benki hiyo  la Shinda Babkubwa na Ecobank Bw. Ipyana Mwakasaka kutoka Tegeta, Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa sekta ya Umma Ecobank Ndabu Swere na Kutoka kushoto ni mshindi wa Shindano la Shinda Babkubwa na Ecobank Bw. Ipyana Mwakasaka, Mkuu wa Bidhaa na Masoko Ecobank Andrew Lyimo, Mkuu wa Domestic Banking Joyce Malai.

 

Posted On Thursday, 14 February 2013 03:01

IMG-20130213-00858 01c4a

Posted On Wednesday, 13 February 2013 16:14

 0006 MWEI 6d889

 

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mrisho Gambo akimkabidhi Hadija Tengeza wa kijiji cha Kwa Mndolwa mkopo wa Mwei kutoka Vodacom Foundation uliowanufaisha wanawake wajasariamali zaidi ya 90 wa kijijini hapo. Wengine picha kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Korogwe Martha Munuo, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Afisa wa Vodacom Foundation Ally Mbuyu na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(kulia).

 

Mpango mahsusi wa kampuni ya Vodacom wa kuwawawezesha wanawake wajasiriamali wadogo kiuchumi vijijini umeendelea kutoa tumiani kwa jasiriamali zaidi wanawake ambao ukuzaji wa mitaji ya biashara wanazoziendesha  sio wa uhakika kutokana na kukosa uwezo wa kukopesheka kutoka  taaisi za fedha. Ikiwa tayari imeshawanufaisha wanawake zaidi ya 7,000 nchini mradi wa Mwei

Posted On Wednesday, 13 February 2013 06:39

pro 0634e

Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo akikabidhi leseni ya uchimbaji madini kwa Bw. Roman Lyaruu kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Itewe wilaya ya Chunya. Mhe. Waziri alisisitiza wachimbaji wa madini kulipa kodi zote zinazotozwa na Mamlaka za Serikali ikiwemo mrabaha wa asilimia nne.

Posted On Tuesday, 12 February 2013 15:18

11 2d0e1

Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja
.Tanzania imefanikiwa kushinda
kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro,
Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla hiyo
imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi,
Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika
ukanda wa Afrika Mashariki

14 a6740

 

Posted On Tuesday, 12 February 2013 07:56

 

9 096b3

 

 

Na: Albert Sanga, Iringa.

Makala haya ninayaandika leo ikiwa ni baada ya kumtembelea Bw. Frank Mwaisumbe nyumbani kwake; jumapili mbili zilizopita na kubadilishana nae mawazo. Bw. Mwaisumbe ni mfanyabiashara aliyepo mjini Iringa anaemiliki kampuni inayohusika na uwakala wa safari za Anga, iitwayo Getterland Company Limited na pia ni mmoja ya waasisi wa shirika la Mindset Empowerment linaloendesha mashindano ya mbio za Ruaha Marathon. Nilimfahamu Bw. Mwaisumbe zamani kidogo na kuna kitu cha kusisimua hapa; kwa sababu ni mwalimu aliyenifundisha kozi ya masoko nikiwa chuo kikuu Tumaini Iringa. Wanablog  mtakumbuka kuwa mara kadhaa nimekuwa nikichambua namna wasomi wetu (wahadhiri, maprofesa na madaktari wa biashara) wanavyokwama kuzalisha wafanyabiashara halisi; kwa sababu wanafundisha mambo ambayo wenyewe “hawayajui kwa vitendo”.(Soma zaidi makala hii)

Posted On Monday, 11 February 2013 06:16
Page 42 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Simu