We have 132 guests and no members online

×

Warning

JUser: :_load: Unable to load user with ID: 641

DSC00454 8737c

 

Na: Albert Sanga

Ninafahamu kuwa linapokuja suala la matumizi ya lugha ya Kiswahili katika mambo ya biashara na ujasiriamali-akili zetu zinapwaya. Sio kwa sababu Kiswahili hakina maneno yote ya kibiashara, la hasha! Lakini ni kwa sababu hatujazoea biashara kwa hiyo misamiati haijatukaa sana kama ilivyotukaa ile ya kisiasa. Moja ya neno hilo ambalo nimeamua kulikopa kama lilivyo ni “Risks”; na ndio dhana nitakayoijadili leo

Kiukweli ujasiriamali unahitaji mtu kuwa na roho ya paka (roho ngumu na ya uvumilivu mkubwa). Leo kupata faida na kesho hasara ama....

Posted On Friday, 18 January 2013 06:11

Shein Pix

            Na: Ali Issa-Maelezo Zanzibar 

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuongoza Mkutano wa saba wa Baraza la Biashara Zanzibar utakaofanyika Jumamosi Januari 19 katika ukumbi wa Salama Hoteli Bwawani mjini Zanzibar.

 Akitoa taarifa kwa Vyombo vya habari huko Gulioni katika Jengo la ZSTC Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Ali Haji Vuai alisema mkutano huo wa saba utazikutanisha

Posted On Friday, 18 January 2013 02:19

1- Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasiisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akifunga kongamano la Ulimwengu la afya ya Uzazi mjini aru 84612

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisisi ya WAMA , Mama Salma Kikwete akifunga kongamano la Ulimwengu la Afya ya Uzazi la  siku 3 Katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa AICC mjini Arusha leo, Kongamano hilo lilewashirikisha wataalamu wa masuala ya afya ya  uzazi wapatao 800 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni,

                                      (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Posted On Thursday, 17 January 2013 13:57

4 09c98

Makatibu wakuu wa Zanzibar wakiwa katika Semina yapamoja kuhusu Kazi na Wajibu wa Tume ya Sayansi na Teknologia iliyotayarishwa na Tume hiyo huko Makumbusho ya Kasri Forodhani mjini Zanzibar.

                              Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

Posted On Thursday, 17 January 2013 13:27

 

Mstaiki meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula na ujumbe wa kamati yake ya fedha wametembelea halmashauri ya manispaa ya Ilala kwa maagizo ya Mhe.Waziri Mkuu kuja kujionea mbinu za kisasa za kukusanya mapato. Mstaiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa amewakaribisha na kuwaeleza jinsi walivyoweza na wanavyoendelea kukusanya mapato.

Posted On Thursday, 17 January 2013 09:23

 

                                                Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi

 

Na: Gladness Mushi Arusha

SERIKALI kwa kushirikiana na wadau inaendelea kutekeleza mpango wa miradi ya miaka mitano wa kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga wakati wa kujifungua na walio chini ya miaka mitano ikiwa ni hatua ya kuboresha huduma ya mama na mtoto na kuokoa maisha yao.

Posted On Thursday, 17 January 2013 04:54

 

Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Dar es Salaam wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda cha Bia cha TBL Arusha, Ben Mwanri (wa pili kushoto), walipotembelea Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, wakati wa  ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.

Posted On Wednesday, 16 January 2013 15:46

Picha na 1 9a7cc

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza kwa wajumbe wa mkutano wa tathmini ya mbio za Mwenge mwaka 2012 kuhusu serikali kufuatiliaji  maendeleo ya miradi inayozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge mjini Zanzbar.

Posted On Wednesday, 16 January 2013 14:13

3 e4c4b

Na: Heka Paul- Maelezo

Shirika la Fedha Duniani(IMF) limepomngeza Tanzania kwa usimamizi mzuri wa kisera ambao umesaidia utulivu wa kiuchumi ambao umesaidia kuleta matumaini hatua iliyosababisha mfumuko wa uchumi hapa nchini kuendelea kushuka.

Posted On Tuesday, 15 January 2013 14:04

1 48eb0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa siku tatu wa kuboresha  Afya ya Mama na Mtoto, ulioanza leo Januari 15, 2013, jijini Arusha. Picha na OMR

Posted On Tuesday, 15 January 2013 13:15

 

 

 

dsc00559 8ce19

 MGOGORO wa vizimba katika soko la wafanyabiashara wadogo la Machinga Complex lililoko jijini Dar es Salaam umeingia hatua nyingine baada ya Meneja wa soko hilo, Nyamsukura Masondore kuvamiwa na wafanyabishara hao, kumpiga hadi kumvunja mkono.

Posted On Monday, 14 January 2013 10:09

 Nikiwa kama mjukuu kipenzi wa bibi yangu, huwa napenda sana kutumia muda wangu wa mapumziko kujadiliana naye mambo mbalimbali yanayohusu jamii, iwe yaliyokuwa yanatokea hapo awali au yanayoendelea kutokea. Ilikuwa ni siku ya jumapili baada ya kutoka kwenye mihangaiko, niliingia ndani na kumuita bibi kwa jina lake la utani ‘Nyaksi’ ili twende nje tukapunge upepo na mazungumzo ya hapa na pale.

   Kama ilivyo ada yangu, huwa napenda sana kutafiti mambo mbalimbali, nikamuuliza bibi, eti bibi nimewahi kusikia kuwa wakati wa enzi zenu mlikuwa hamruhusiwi kula mayai wakati wa ujauzito kwa kuwa mtoto atazaliwa bila nywele? Bibi Nyaksi huku akitabasamu akanigeukia na kusema, "umeshaanza, kwanza usikumbushe enzi zile bado nipo mbichi" akimaanisha wakati yupo msichana. Wote tukatabasamu kwa pamoja. Nyaksi akaendelea kusema sio mayai tu, bali vyakula vyote nyenye virutubisho kwa wingi ambavyo ninyi vijana wa leo mnaviita ‘purotini’, akiitamka protini kwa lafudhi ya kizee. Nyaksi alisema tulizuiliwa kula vyakula hivyo kwa mlengo wa mwiko, akaendela kusema, unajua Babu (jina langu alilopenda sana kuniita Nyaksi) wazee walitumia mwiko ili kututisha lakini ukweli ni kuwa wakati ule hakukuwa na tekenolojia (akimaanisha teknolojia) hivyo kama utakula vyakula vyenye virutubisho sana vitamfanya mtoto awe mkubwa, na hivyo kama utashindwa kujifungua kwa njia ya kawaida basi hakutakuwa na njia nyingine ya kukusaidia. Nyaksi akaendelea ninyi vijana wa siku hizi mna raha, hospitali nyingi, madaktari wengi huku mna njia nyingi mbadala ikiwemo ya upasuaji na nyinginezo. 

Posted On Monday, 14 January 2013 04:11
Page 46 of 48

Tafuta Habari

Blog Shabihana

Smart